Michirizi Ya Damu – 10

“Nisamehe mpenzi! Nilikuwa sehemu fulani hivi,” alisikika Mickey kwenye simu.

“Nimekukumbuka jamani! Mpaka nikataka nijiue kwa ajili yako,” alisema Fareed kwa sauti yake ya kuwapagawisha wanaume.

Wakazungumza mengi na mwisho wa siku wakakubaliana kwamba lingekuwa jambo jema kama wangekutaka katika Klabu ya Dubai Night kwa ajili ya kuburudika na kuzungumza mengi. Hiyo ilikuwa furaha kwa Fareed kwani kitu pekee alichokuwa akikitaka kwa kipindi hicho ni kuonana na mwanaume huyo tu.

“Nakuja bebi!”

“Sawa.”
Akakata simu. Akaelekea bafuni na kujiandaa. Siku hiyo alijiapiza kwamba ni lazima alale na Mickey kwani kama asingefanya hivyo basi kungekuwa na watu ambao wangemfuata na kulala naye kisha kumsahau yeye.

HAkutaka kuona hilo likitokea. Alichukua dakika kumi kuoga, akatoka bafuni na kisha kuanza kujipaka losheni na kujipulizia marashi yake ya Kizenji, alipomaliza, akavaa taiti iliyombana hasa iliyokuwa na rangi nyeusi, akakibusti kifua chake na kisha kupaka wanja sehemu nyusi zake alizokuwa amezinyoa na kumalizia na kujipata lipstiki mdomoni.

Alipojiangalia kwenye kioo, yeye mwenyewe akajitamani, siku hiyo alitoka chicha, alikuwa akivutia na aliamini kwa kila mwanaume ambaye angemuona, kusingekuwa hata na mtu mmoja ambaye angegundua kwamba alikuwa mwanaume kwani alikuwa na muionekano wa kike kwa asilimia mia moja.

Akatoka mpaka nje ya hoteli ambapo ndani ya dakika chache, Mickey akafika mahali hapo na kumchukua. Ndani ya gari kila mmoja alionekana kuwa na furaha tele. Ilikuwa vigumu kumgundua Mickey kwamba alikuwa na mpango mchafu kwani kwa jinsi alivyokuwa akitabasamu, ilionekana kabisa hakukuwa na tatizo lolote lile.

HAwakuchukua muda mrefu wakafika klabu ambapo wakateremka na kuelekea ndani. Humo, Fareed alionekana kama kuchanganyikiwa, alikuwa akicheza kila wimbo uliokuwa ukipigwa na kila alipotaka kunywa, alikwenda sehemu ya kununulia vinywaji na kunywa kwani alikuwa na mtu mwenye pesa.

Wakati hayo yote yakiendelea, vijana wa Keith walikuwa humo ndani, walikuwa wakifuatilia kila kitu, walimwangalia, wao wenyewe walihisi kwamba alikuwa mwanamke kwa jinsi alivyokuwa amejiremba na kuonekana mrembo kupita kawaida.

Muziki uliendelea mpaka iipofika saa tisa ambapo wakatoka huku Fareed akiwa amechoka kupita kawaida. Wakaingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo.

Wala hawakuchukua mwendo mrefu, Mickey akasimamisha gari pembezoni mwa barabara ambapo hakukuwa na mwanga mkali na kisha kuteremka, Fareed alishangaa, naye akateremka kwa kuhisi kulikuwa na kitu lakini hata kabla hajafanya kitu chochote kile, gari moja likasimama, wanaume wawili waliokuwa na miili mikubwa wakateremka, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumfuata, wakamkamata na kumziba mdomo kisha kumuingiza ndani ya gari lao na kuondoka.

Fareed aliogopa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendela, hakujua wale watu walikuwa wakina nani na kwa sababu gani walikuwa wamemteka kama walivyofanya.

Wakati akijiuliza hilo, mwanaume aliyekaa pembeni ya dereva akageukia kule nyuma na kumwangalia Fareed, walipogonganisha macho, akashtuka baada ya kugundua kwamba alikuwa Keith.

“Keith…” aliita Fareed.

“Yes my love!” (ndiyo mpenzi wangu) alisema Keith huku akitoa tabasamu.

“What are you doing?” (unafanya nini?)

“I just want to play a game! A nice one, it is Flecks of Blood,” (ninataka tucheze mchezo! Mchezo mzuri, unaitwa Michirizi ya Damu) alijibu Keith huku akiwa kwenye tabasamu pana.

Safari iliendelea, Fareed alikuwa na hofu kubwa moyoni mwake, alijua kabisa kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, hakutegemea kuona mwanaume huyo akimfuatilia mpaka huko.
Akaanza kuomba msamaha kwa kuamini kwamba angesamehewa lakini hicho hakikuwa kipindi cha kusamehewa bali kilikuwa kipindi cha kuuawa kwa kile alichokuwa amekifanya.

Gari likaondoka na kuelekea katika ufukwe wa Kite, huko, tayari kulikuwa na boti waliyokuwa wameiandaa ambayo ingewapeleka mpaka mbali kabisa kwa ajili ya kumtosa baharini, na hawakutaka kabisa mwili wake uonekane, hivyo walikuwa na jiwe ndani ya boti ile kubwa.

Wakateremka na kuingia ndani ya boti na safari ya kuelekea katikati ya bahati kuanza. Njiani, kila mtu alikuwa akimwangalia Fareed kwa macho yaliyojaa tamaa, kwani kwa jinsi alivyokuwa, ilikuwa vigumu sana kumuacha hivihivi.

Hapo ndipo walipoanza kumbaka kama walivyokubaliana. Fareed alisikia maumivu makali, alikuwa akilia huku akitaka kuachwa lakini hakukuwa na mtu aliyekuwa radhi kumuachia.

Aliendelea kubakwa mpaka akahisi mwili ukikosa nguvu, macho yake yakaanza kujaa giza, na hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.

“Tayari! Mfungeni jiwe,” aliagiza Keith, Fareed akafungwa jiwe kubwa na kisha kutupwa baharini. Akaanza kuzama huku akiwa amepoteza fahamu. Walichokifanya wanaue hao, kwa haraka sana wakaondoka mahali hapo huku kila mmoja akiwa na furaha kwani waliamini kwamba kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angeuona mwili wa Fareed.

****

Asteria alichanganyikiwa, hakujua mahali alipokuwa Fareed, alijaribu kumtafuta katika simu yake kwa kuona kwamba angempata na kuwasiliana naye kwa ajili ya biashara lakini mwanaume huyo hakupatikana.

Hakujua alikuwa wapi, aliangalia kwenye WhatsApp yake, ilionyesha kwamba mara ya mwisho kwa mwanaume huyo kuwa katika mtandao huo ilikuwa ni wiki moja iliyopita.

Hakujua ni kwa jinsi gani angempata, akajaribu kuwasiliana na Keith na kumuuliza kuhusu Fareed lakini bilionea huyo alimwambia kwamba yeye mwenyewe alikuwa akimtafuta kwani alimuaga kwamba anakwenda Dubai, baada ya hapo hakumuona tena.

Hakumwambia ukweli kwamba alimuua Fareed, alimficha kwa kuhisi kwamba siri hiyo ingedumu milele. Moyoni mwake hakuwa na huruma, kwa kile alichokifanya kwake kilionekana kuwa sahihi kwani kama kuumizwa moyo wake na mwanaume huyo, aliumizwa sana na hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kumuua bila huruma.

Asteria hakutaka kukubali kuendelea kubaki nchini Tanzania, Fareed ndiye alikuwa biashara yake kubwa, japokuwa alikuwa na wanawake wengine waliokuwa wakijiuza lakini kwa mwanaume huyo ndiye alikuwa soko, aliyempa pesa na kuishi katika maisha ya raha kupita kawaida.

“Nakwenda Dubai!” alisema Asteria.

“Kufanya nini?”
“Kumtafuta Fareed.”
“Kwani bado hujampata?”
“Ndiyo! Wewe umempata?”
“Hapana!”

Alikuwa akizungumza na mmoja wa wasichana waliokuwa wakimfanyia kazi. SIku iliyofuata, hakutaka kubaki nchini Tanzania, akapanga safari na kupaa kuelekea Dubai kwa kuamini kwamba angeweza kumuona huko.

Moyo wake ukaanza kuingiwa na hofu, akahisi kwamba mwanaume huyo alikuwa amekufa na mwili wake kutupwa kwani kwa mtu kama Fareed, jinsi alivyokuwa akipenda mitandao ya kijamii lingekuwa suala gumu sana kukaa hata saa moja pasipo kuingia Facebook, WhatsApp, Beashare au mtandao mwingine wowote ule.

Alipofika Dubai, akaelekea hotelini. Siiku hiyo hakuwa sawa, alipanga kuonana na wanawake wengine ambao walikuwa chini yake, akaonana nao na kuzungumza nao pamoja na kuwauliza kuhusu Fareed lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akifahamu mahali alipokuwa, kila mmoja alisema kwamba mara ya mwisho kumuona ilikuwa ni kabla hajakwenda Ubelgiji, baada ya hapo hawakujua alikuwa wapi.

Alikaa Dubai kwa mwezi mzima, hakumuona Fareed na wala hakujua mahali alipokuwa. Akakata tamaa na kuona kwamba tayari mwanaume huyo alikuwa marehemu hivyo kitu pekee alichokuwa akikitaka ni kuiona maiti yake ili ajiridhishe tu.

“Hata nikiiona maiti yake nitashukuru Mungu! Yaani Fareed amekufa? Amekufaje? Mbona hata taarifa sikupewa?” alijiuliza huku akiwa amechanganyikiwa, hakujua kabisa mahali alipokuwa mtu huyo.

Alichokifanya ni kuwasiliana na marafiki zake wengine waliokuwa wakiishi nchini humo na kuwaambia kile kilichokuwa kikiendelea kwamba kulikuwa na ndugu yake ambaye hakujua mahali alipokuwa mpaka muda huo, hao ndiyo waliomshauri kwamba alitakiwa kutembelea katika hospitali mbalimbali kwa ajili ya kumtafuta kwani inawezekana alikuwa amekufa ila mwili wake ulihifadhiwa mochwari.

Hilo lilikuwa wazo zuri, alichokifanya siku iliyofuata ni kwenda katika hospitali mbalimbali lakini kote huko hakuweza kuukuta mwili wa Fareed kitu kilichomfanya kumalizia katika hospitali ya mwisho ya Sultan Idris Medical Center iliyokuwa pembezoni mwa Dubai ambapo haikuwa mbali kutoka baharini.

Alipofika huko akajitambulisha na kitu kilichomfanya kufika mahali hapo. Kwa jinsi alivyokuwa akijielezea, kila mmoja alimuonea huruma hivyo kumchukua na kuondoka naye kuelekea mochwari kwa ajili ya kuitambua maiti ya ndugu yake aliyokuwa akiitafuta.

“Ni tangu lini?” aliuliza daktari.

“Mwezi mmoja sasa umepita sijaweza kumuona.”
“Una uhakika kwamba alikuja Dubai?”
“Ndiyo! Mara ya mwisho kuwasiliana naye alikuja huku,” alijibu Asteria.

Hawakuchukua mwendo mrefu wakafika katika mochwari ya hospitali hiyo na hivyo kuingia ndani. Humo ndani kulikuwa na masanduku mengi ambayo ndani yake kulikuwa na maiti kadhaa huku kukiwa na baridi kali ambalo muda mwingi Asteria alikuwa akitetemeka tu. Wakaanza kuzunguka huku na kule, wakayafungua madroo makubwa na kuangalia ndani kama kulikuwa na maiti ya Fareed.

Walizunguka kwenye madroo mengi lakini hawakufanikiwa kuiona maiti ya Fareed kitendo kilichomfanya kuhisi kwamba mwanaume huyo hakuwa amekufa lakini wakati akijiandaa kutoka ndipo akaambiwa kwamba kulikuwa na sehemu nyingine ya madroo hawakuwa wameangalia hivyo wakaelekea huko.
Walipofika, yakafunguliwa na kuanza kuangalia maiti moja baada ya nyingine. Muda wote mapigo ya moyo wake yalikuwa juu, kila alipopiga hatua alikuwa akitetemeka mno.

Baada ya dakika kadhaa, wakafika katika droo moja kubwa, ndani yake kulikuwa na maiti ya mwanaume mmoja, ilikuwa imefunikwa, haraka sana msimamizi aliyekuwa ndani ya mochwari ile akaifungua maiti ile, macho ya Asteria yalipotua katika sura ya maiti ile, miguu yake ikamlegea, hakuamini kile alichokiona, akashindwa kuvumilia, hapohapo akaanza kulia kama mtoto.

***

Bilionea Keith alikuwa mwenye furaha tele, alichokuwa akikitaka alitekeleza, moyo wake ulikuwa na faraja kubwa, alijona shujaa kwani kitendo cha kuchunwa pesa zake na mtu ambaye baadaye alikuja kumsaliti, kwake ilionekana kuwa dhambi kubwa.

Alikunywa na kuyafurahia maisha yake, kila alipokaa baa na kunywa pombe, akili yake ilikuwa kwa Fareed ambaye alimchukia kupita kawaida. Moyo wake haukujuta hata mara moja, alijipongeza kwa kazi kubwa aliyokuwa ameifanya.

“Mungu mlaze mahali pema peponi,” alisema Keith huku akiinua glasi ya pombe yake juu.

Wiki ya kwanza ikakatika, ya pili ikaingia, hakuacha tabia yake ya kuchukua wanawake. Alikuwa akipenda wanawake kama alivyokuwa akipenda kula. Alikuwa na familia yake, aliipa kila kitu lakini kamwe hakuacha tabia yake ya kulala nje. Alijua kwamba mkewe aliumia sana lakini hakutaka kujali, kwake, kulala na wanawake wengi ndiyo yalikuwa maisha yake.

Akili yake ni kama ilikuwa imevurugwa, wanawake walimpagawisha kupita kawaida. Akili ikaathirika kwa wanawake, hakuwa akifanya kitu chochote pasipo kufikiria ngono.

Alitembea nchi nyingi, huko alilala na wanawake wengi, alitembea nao pasipo kuhofia kitu chochote kile. Wakati akiwa katika harusi ya rafiki yake iliyokuwa ikifanyika nchini Malaysia, ndipo akakutana na msichana mrembo, mwenye sura yenye mvuto, msichana huyo mweusi aliyekuwa raia wa Nigeria akatokea kumpagawisha kupita kawaida.

Hakutaka kuchelewa, moyo wake ulichanganyikiwa, kwa jinsi alivyomwangalia mwanamke yule, alisikia damu yake ikizunguka kwa kasi kubwa katika mishipa yake.

Hakutaka kuchelewa, kwa haraka sana akamsogelea, alipomfikia, akamsalimia, msichana huyo alipoitikia, sauti yake ikamuingia mpaka moyoni mwake, ikaivuruga akili yake, tabasamu lake likamburuza vilivyo.

“You look very beautiful,” (unaonekana mrembo sana aiseee) alisema Keith huku akiachia tabasamu pana.

“You too my babyto…” (wewe pia mpenzi wangu) alijibu msichana huyo huku akitoa tabasamu pana, Keith alipoangalia meno, akagundua kwamba msichana huyo alikuwa na mwanya mdogo, huo ndiyo ulikuwa ugonjwa wake mkubwa.

“My name is Keith from Los Angeles…” (naitwa Keith kutoka Los Angeles…) alijitambulisha harakaharaka huku akimpa mkono.

“Maria Ogabugu from Lagos…” (Maria Ogabugu kutoka Lagos…) alijibu msichana huyo huku akimpa mkono. Walipogusana tu, Keith akahisi kama akipigwa na shoti ya umeme. Kwa kifupi, kwa Maria, alikufa na kuoza, hakutaka kuambiwa chochote kile.

“I like Africa…” (naipenda sana Afrika) alisema huku akiachia tabasamu pana.

****

Ulikuwa ni msimu wa joto kali Mjini Dubai, katika kipindi hicho watu wengi waliokuwa wakiishi huko waliondoka na kuelekea katika nchi nyingine kutokana na hali hiyo kuwatesa sana.

Nyuzi joto ambayo kila siku iliwaonyesha kwamba ni nyuzijoto 34 ilibadilika mpaka kufika nyuzijoto 42. Hali ilitisha na hata wale waliokuwa ndani ya nyumba zao, muda wote ni viyoyozi tu ndiyo vilivyokuwa vikiwapuliza.

Katika kipindi hichohicho cha joto kali ndicho kipindi ambacho hakukuwa na mwezi angani, baharini kulikuwa na giza, hata wale wavuvi ambao walikuwa wakiondoka kwenda kuvua, hawakwenda mbali, kwa kutumia taa zao, samaki walifuata mwanga na kuwavua kirahisi zaidi.

Katika kipindi hichohicho cha joto kali na giza kubwa baharini ndicho kilikuwa kipindi ambacho mvuvi maarufu wa samaki, mzee Ahmedi El Saadat aliuchukua mtumbwi wake na kwenda baharini kwa ajili ya kuvua samaki kama alivyokuwa akifanya siku nyingine.

Alipofika mbali, akashusha nyavu zake na kuanza kusubiri samaki. Alikaa mahali hapo, siku hiyo kulikuwa na giza kubwa, siku hiyo ilionekana kuwa ya tofauti kwake kwani alikuwa na hofu moyoni mwake mpaka wakati mwingine akahisi kwamba kungekuwa na tatizo lingetokea mahali hapo.

Alikaa kwa nusu saa, ghafla akaanza kuisikia boti kubwa ikienda kule alipokuwa. Alishtuka, alihisi wale walikuwa watu wabaya ambao walitaka kumfanyia kitu kibaya mule baharini, boti ile ya kifahari ilikwenda na kusimama mbali kabisa ambapo ghafla akawaona watu wakitoka huku wakiwa na mtu mwingine aliyekuwa akilia kuomba msamaha.

Aliogopa, akajua kwamba hao hawakuwa watu wazuri hata kidogo, alibaki akiwaangalia, hakujua walitaka kufanya nini, kwa jinsi mtu yule alivyokuwa akilia, aligundua kwamba lengo kubwa lililowafanya kufika mahali hapo lilikuwa ni kumuua tu.

Huku akiwa haamini macho yake, watu wale wakaanza kumbaka mtu waliyekuja naye, aliumia moyoni mwake, moyo wake ukajawa na hasira, alitamani sana kuwafuata na kupambana nao, alijua ni kwa jinsi gani Mungu aliyekuwa akimwabudu alikataza vitu kama hivyo, alisaga meno lakini akajificha zaidi kwani alijua kwamba kama angefanya chochote na kuonekana, basi angeuawa kama kupoteza ushahidi.

Kitendo cha kumbaka Fareed kilichukua dakika nyingi mpaka alipozimia ambapo wakamchukua, wakamfunga kamba ngumu iliyokuwa na jiwe kisha kumtupa baharini na kuondoka mahali hapo.

Alisubiri mpaka wafike mbali ndipo akajitosa baharini. Hakutaka kuona mtu huyo akifa mbele ya macho yake, moyoni mwake alijisikia hukumu nzito hivyo ilikuwa ni lazima amsaidie kwa nguvu zote kumuokoa kwenye kifo kilichokuwa kikimsubiri.

Akazama kwenye maji huku akiwa na kisu chake alichokuwa akikitumia kuparuria samaki. Alipofika chini na kumulika kwa tochi yake, akafanikiwa kumuona Fareed akiwa chini kabisa, amenasa kwenye tope huku akiwa hajitambui kabisa.

Akamfuata mpaka pale alipokuwa na kuanza kuikata kamba ile ambayo wala haikumletea ubishi sana, ikakatika na kisha kumchukua na kuanza kwenda naye juu.

Alifanikiwa, alipofika kwenye boti yake ndogo, akamchukua na kumuweka kisha kuanza kumtoa maji yaliyoingia mwili mwake. Hilo lilionekana kumsaidia, alipomaliza, akawasha boti na kuondoka, hata kuendelea kuvua samaki mahali pale, hakutamani tena.

Alipofika ufukweni, akalifuata gari lake ambalo kila siku alikuwa akija nalo na kulipaki sehemu, akamuingiza Fareed na kuondoka mahali hapo huku akiwa anapiga dua kimoyomoyo kama kumtaka Mungu amponye mtu aliyekuwa naye, hakumfahamu ila moyo wa huruma ulimuingia na kuamua kumsaidia kwa moyo mmoja.

Alipofika nyumbani akamuingiza ndani na kumlaza kitandani. Kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alikuwa akijiuliza kuhusu Fareed, alikuwa msichana au mvulana.

Alikuwa na muonekano wa kike, ila alipoiangalia vizuri mikono yake, akagundua kwamba alikuwa mwanaume, sasa mwanaume gani aliyekuwa na muonekano huo?

Alijazia kwa nyuma, alikuwa na kifua kikubwa, matiti yaliyosimama, kwa kifupi alichanganyikiwa na hakujua kuhusu mtu huyo, kwake, alikuwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu yake.

Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, akamvua nguo na kumwangalia sehemu za siri, yeye mwenyewe alichanganyikiwa, alikuwa na muonekano wa msichana mrembo lakini kumbe sehemu zake za siri zilikuwa ni za mwanaume.

“Huyu ni nani?” alijiuliza.

Mkewe akaingia chumbani humo, akamfuata mumewe na kumuuliza kuhusu mtu huyo. Hakumficha, alimwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea, jinsi alivyowaona watu wabaya wakimtupa baharini kwa lengo la kumuua, lakini kwa kuwa aliwaona, akaenda kumuokoa akiwa amezamishwa ndani ya maji.

“Alhamdulilah!” alisema mkewe huku akiangalia juu na kuinua mikono yake kama ishara ya kumshukuru Mungu.

Hapo ndipo alipoanza kupata matibabu, katika kipindi chote hicho, mke wa mzee aliyekuwa Ahmedi hakuwa akijua kama mtu aliyepelekwa nyumbani kwake na mumewe alikuwa mwanaume, alikuwa na muonekano wa asilimia mia moja wa kike.

Aliharibika vibaya kwa nyuma, mzee Ahmedi aliligundua hilo lakini hakutaka kumwambia mke wake, alikuwa kimya huku wakati ambao mwanamke huyo hakuwepo nyumbani, alichukua nafasi hiyo kumtibu nyuma kulipoharibika vibaya.

Waliendelea kumuhudumia nyumbani hapo mpaka siku mbili baadaye aliporudiwa na fahamu. Kitu cha kwanza kabisa baada ya kufumbua macho ni kuanza kuangalia huku na kule, alishangaa mahali alipokuwa, hakukumbuka chochote mpaka alipotulia kwa dakika kadhaa na kukumbuka kile kilichokuwa kimetokea kabla ya kuwa mahali hapo.

Moyo wake ulimuuma mno, hakuamini kama kweli Keith alimfanya hivyo, moyo wake uliumia, alitakiwa kuuawa lakini aliokolewa na mwanaume huyo mvuvi ambaye alimwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea.

Fareed hakutaka kuondoka nyumbani hapo, alitulia, wiki moja baadaye alipojisikia afadhali, akaaga na kuondoka zake kurudi nchini Tanzania. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, kifua chake kikajaa kisasi, hakukuwa na kitu kilichomuumiza kama kubakwa na vijana wa Keith ambaye hakuridhika na kutaka kumuua.

Alipofika nchini Tanzania, ndani ya Jiji la Dar es Salaam, akaelekea nyumbani kwake ambapo huko akampigia simu Asteria, baada ya kusikia sauti ya Fareed hakuamini, akamwambia kwamba angekwenda nyumbani hapo kuzungumza naye, alitaka kujua ni kitu gani kilitokea.

Ndani ya dakika thelathini tu mwanamke huyo alikuwa ndani ya nyumba hiyo, alimkumbatia Fareed, hakuamini kama mwanaume huyo alikuwa hai, alijua kwamba alikufa.

“Nilikufuata mpaka Dubai,” alisema Asteria.

“Ikawaje?”
“Nilikwenda hospitali na kuonyeshewa miili mingi. Niliiona maiti ya Ashura ndani ya kabati kubwa mochwari,” alisema Asteria maneno yaliyomshtua Fareed.

“Ashura?”
“Ndiyo! Nilishtuka sana, sikuamini macho yangu. Fareed, iliniuma sana. Hebu niambie na kwako ni kitu gani kilitokea?” aliuliza Asteria huku akimwangalia Fareed.

“Ni mambo makubwa yaliyonitokea. Hakika nitamchukia Keith maisha yangu yote,” alisema Fareed huku akimwangalia Asteria.

“Kuna nini tena?”

ITAENDELEA KESHO

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment