The House of Favourite Newspapers

Miili ya Wanajeshi Waliouawa DRC Kurejeshwa Nchini Leo

Luteni Jenerali James Mwakibolwa.

Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa Taarifa kwa Umma kuwa, Askari wake waliouawa na waasi wakilinda amani katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) itawasili nchini leo, Jumatatu.

 

Taarifa ya Ofisi ya Habari ya JWTZ imesema miili ya askari hao itawasili nchini leo Jumatatu Desemba 11,2017 saa 12 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.

 

Awali, akizungumzia na waandishi wa habari jana Jumapili Desemba 10, 2017, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema miili ya askari hao ingerejeshwa nchini kati ya Jumanne Desemba 12, au Jumatano Desemba 13,2017 kwa ushirikiano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa (UN).

 

Jenerali Mwakibolwa alisema askari hao walivamiwa kambini na waasi wa ADF na mapigano yalidumu kwa takriban saa 13. Alisema askari 14 wa JWTZ waliuawa, 44 wamejeruhiwa na wengine wawili  hawajulikani walipo.

 

Tukio hilo lililotokea Desemba 7,2017 katika Kambi Ndogo iliyopo katika Daraja la Mto Simulike, kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu nchini DRC.

 

UKAWA WATISHIA KUSUSIA UCHAGUZI WA JANUARI 13, ENDAPO SERIKALI HAITAFUATA HAYA (VIDEO)

Comments are closed.