The House of Favourite Newspapers

Milipuko Yatikisa Ngome ya Urusi Iliyopo Crimea, Yadaiwa Kuwa Mapigo ya Makusudi

0
Mlipuko Crimea

CRIMEA Peninsula ambayo ilitekwa kutoka Ukraine na kisha kutwaliwa na Urusi mapema 2014, na wakati majeshi ya Urusi yalipoanzisha uvamizi mpya kwa Ukraine mwezi Februari walitumia  ngome zao za Crimea kukamata maeneo makubwa ya kusini mwa Ukraine.

 

Maafisa wa Urusi walisema mlipuko huo ulisababisha na moto katika eneo la kutupia silaha eneo la Dzhankoi kaskazini mwa Crimea, moto pia ulionekana kwenye kituo kidogo cha umeme eneo hilo.

Kiongozi wa Kitaifa wa Crimea amedai kuwa shambulio hilo ni la makusudi kutoka kwa vikosi vya Urusi

Kilichosababisha moto huo bado hakijulikani, lakini wiki iliyopita ndege za kivita za Urusi ziliharibiwa katika shambulio dhahiri la Ukraine kwenye pwani ya Crimea ambapo mshauri wa Ofisi ya Raisi wa Ukraine Mykhailo Podolyak alielezea tukio hilo kama “kuondoa wanajeshi”, akionyesha kuwa milipuko hiyo haikutokea kwa bahati mbaya.

 

Kiongozi wa Kitaifa wa Crimea, Refat Chubarov, pia alielezea milipuko hiyo kama pigo la makusudi na sio kwa bahati mbaya.

Crimea ni eneo linalotawaliwa na vikosi vya Urusi

Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema moto huo ulizuka katika eneo la kuhifadhia risasi karibu na kijiji cha Maiske muda wa saa 06:15 kwa saa za Moscow na kwamba chanzo kinachunguzwa.

 

Imeandikwa: John Mbwambo kwa msaada wa mitandao.

 

 

 

Leave A Reply