The House of Favourite Newspapers

Waziri Nape Azindua Mawasiliano ya Intaneti yenye kasi Mlima Kilimanjaro

0
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye

LEO Agosti 16, 2022 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amezindua rasmi mawasiliano ya intaneti yenye kasi katika mlima mrefu kuliko yote Afrika Mlima Kilmanjaro.

 

Ufikishwaji wa huduma hii umewezeshwa na shirika la mawasiliano Tanzania TTCL lililofikisha huduma hii katika mlima Kilimanjaro katika utekelezaji na maboresho ya mkongo wa taifa wa mawasiliano wenye lengo la kufikisha mawasiliano ya intaneti ya uhakika katika maeneo yote ya Tanzania.

 

Akiongea wakati wa hafla fupi kabla ya uzinduzi rasmi Mkurugenzi mkuu wa TTCL Peter Rudolph Ulanga alisema:

Waziri Nape akizindua mtandao wa intaneti mlima Kilimanjaro

“Katika utekelezaji na maboresho ya mkongo wa taifa wa mawasiliano

Shirika litapeleka huduma za mkongo wa taifa la mawasiliano katika maeneo yote ikiwemo maeneo ya vivutio vya utalii.

 

Mpaka sasa huduma hii ya mawasiliano katika mlima Kilimanjaro imefika katika kituo cha Mandara, horombo na kibo huku lengo ni kufikisha huduma hii katiaka kilele cha Mlima katika kituo cha Uhuru mita 5895 kutoka usawa wa bahari, hii itakuwa ni sehemu ya juu Zaidi kufikishiwa mawasiliano ya mkongo wa taifa Afrika na Duniani kwa ujumla.

 

Mradi umegharimu mil 146 na utasaidia kurahisisha mawasiliano na kuijenga Tanzania ya kidigitali.”

Mradi umegharimu pesa za kitanzania shilingi Milioni 146

Aidha Waziri Nape aliongeza kwa kusisitiza umuhimu wa uwepo wa huduma hii katika mlima Kilimanjaro pamoja na kupongeza juhudi za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuboresha miondombinu itakayoleta maendeleo kwenye taifa hili.

 

“Awali shughuli za utalii ziikuwa zikifanyika bila huduma za mawasiliano, hali hii ilikuwa ni hatari kwa usalama wa watalii na watoa huduma za utalii. Aidha kukosekana kwa mawasiliano serikali ilikuwa ikikosa mapato na fursa ya kutangazwa Zaidi na watalii watakaoweka picha watakazopiga kwenye mitandao ya kijamii. Kabla ya mwisho wa mwaka huu tunataka tufike uhuru peak tuiambie dunia Tanzania ndipo lilipo paa la Afrika, watalii kati ya 800 mpaka 1000 wataenda kuhudumiwa kila siku.” alisema Waziri Nape.

Imeandikwa: Abdallah Kaputi kwa msaada wa mitandao.

 

Leave A Reply