The House of Favourite Newspapers

MILIPUKO YAUA WATU TAKRIBANI 207 SRI LANKA WAKIWEMO WATALII

Watu wapatao 207 wameuawa kutokana na mfululizo wa mabomu yaliyolipuka kwenye mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo. Polisi imethibitisha kuwa watu wengine zaidi ya 500 wamejeruhiwa

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Ruwan Gunasekera mlipuko mwingine umetokea muda mfupi katika hoteli iliyopo jimbo la kusini mwa Colombo la Dehiwala likiwa ni shambulio la saba kufanyika katika siku hii ya Jumapili. Mlipuko wa nane umetokea kwenye kitongoji cha Orugodawatta kaskazini mwa mji mkuu.

 

Mpaka sasa hakuna yeyote aliyedai kuhusika na mashambulio hayo na wala idara za usalama hazijasema iwapao mashambulo hayo yalifanywa na magaidi.

Lakini kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mashambulio hayo yalizilenga sehemu za kidini na kiuchumi. Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena amesema majeshi ya ulinzi na polisi wameanzisha uchunguzi. Viongozi mbalimbali duniani wamelaaani mashambulio hayo.

Jumapili ya Pasaka ni moja ya siku kuu muhimu sana katika kalenda ya waumini wa dini ya Kikristo.

Hakuna kundi lolote lililojihusisha na mashambulizi hayo.

Kumekua na hofu huenda wapiganaji wa kundi la Islamic State waliorejea kutoka mashariki ya kati wakawa tishio kwa usalama wa nchi hiyo.

Comments are closed.