The House of Favourite Newspapers

Amber Lulu kikaangoni kwa picha chafu

ACHANA na video yake inayosambaa mitandaoni ikimwonyesha msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu akigawa zawadi kwa watoto akiwa amevaa nguo zisizo na staha kwa jamii ya wastaarabu, ukiingia kwenye ukurasa wake wa Instagram utashangaa zaidi.

 

Katika tukio hilo la hivi karibuni ambalo linaelezwa kutokea Shinyanga ambapo msanii huyo alikuwa na ‘tour’ ya kimuziki, Amber Lulu ameonekana akiwa kwenye gari la wazi, akiwa amevaa ‘kanguo’ kanakofanania na sidiria na kuacha sehemu ya kifua chake wazi.

Lakini kwenye ukurasa wake wa Instagram, ametundika picha na video nyingi akiwa nusu utupu, jambo ambalo Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemuweka kikaangoni kwa kuchunguza maadili ya picha na video hizo na kumchukulia hatua endapo itahitajika kufanya hivyo.

 

TUKIO LA SHINYANGA

Amber Lulu akiwa kwenye msafara wake binafsi wa gari la wazi, alionekana akipita katika mitaa mbalimbali huku akishangiliwa na watu wakiwemo watoto waliokuwa wamejaa kando ya barabara.

Baada ya Risasi Mchanganyiko kuona ‘clip’ hiyo yenye ukakasi, lilimsaka msanii huyo na kumuuliza kulikoni apite mtaani akiwa na mavazi ya namna ile, akajibu:

 

“Unajua kitu kimoja ambacho watu wengi hawakijui ni kwamba mimi ni msanii, natakiwa kubadilikabadilika kila siku. Sitakiwi kuwa na mwonekano mmoja tu, hata ukiwaangalia kina Beyonce na Rihana (wanamuziki wa Marekani) ni watu ambao wanabadilika kimuonekano.

“Leo utamuona yuko hivi na kesho yuko vile, hiyo ndiyo maana halisi ya kuitwa msanii. Halafu isitoshe ile nguo mimi niliinunua ikiwa full, juu mpaka chini, sasa siwezi kuvaa na koti juu eti ili nijizibe, sijazoea kabisa hayo mambo. Nashukuru Mungu watoto walifuata pipi nilizokuwa nawagawia na siyo kunitazama mimi.”

 

KIKAAONGONI

Risasi Jumamosi lilimsaka Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza ili kuzungumzia ishu ya msanii huyo kutundika picha na video zisizo na staha kwenye mitandao ya kijamii lakini simu yake haikupatikana.

Hata hivyo, ofisa mmoja ndani ya Basata alipopatikana kuzungumzia ishu hiyo, alisema ni kweli wamekuwa wakiona picha na video za msanii huyo na kwamba wanajipanga kumchukulia hatua.

 

“Hilo jambo anatakiwa kuzungumza katibu (Mngereza ) kwa kuwa yeye ndiye msemaji, lakini ni kweli tumeona na linashughulikiwa kwa mujibu wa kanuni zetu,” alisema ofisa huyo akisisitiza kutoandikwa jina lake gazetini kwa vile siye msemaji.

 

STORI: Memorise Richard, Risasi Jumamosi

Comments are closed.