The House of Favourite Newspapers

Milito: Icardi Kuondoka Ilikuwa Sahihi

STRAIKA wa zamani wa Inter Milan, Diego Milito, ameweka wazi kuwa kuondoka kwa Mauro Icardi kwenye kikosi hicho lilikuwa dili zuri kwa mchezaji yeyote, hivyo kocha Antonio Conte asioneshewe vidole.

 

Icardi aliondoka mwanzoni mwa msimu huu ndani ya Klabu ya Inter na kujiunga na Paris Saint Germain kwa mkopo, huku Inter ikiwachukua Romelu Lukaku na Alexis Sanchez.

 

Milito alisema ana furaha kuona kwa sasa klabu hiyo inafanya vizuri na anaamini itaendelea kuwa hivyo.
“Mauro kwenda PSG lilikuwa ni dili zuri kwake na hata kama angekuwa mchezaji mwingine, huko anafanya vizuri, lakini pia Inter ilipata mbadala sahihi wa kujaza nafasi yake.

 

“Kocha Conte yupo vizuri, sina wasiwasi naye na kwa sasa anaonyesha yeye ni nani ndani ya kikosi hicho.

“Nina furaha pia kuona timu yetu inafanya vizuri na kushinda michezo yake mingi na hilo ndiyo jambo kubwa,” alisema Milito ambaye ni raia wa Argentina.

 

Mwanzoni mwa msimu huu, Icardi aliondoka Inter kujiunga na PSG baada ya kuwa na mvutano na klabu yake hiyo. Milito ambaye amestaafu soka, kipindi chote alichochezea Inter Milan alifunga mabao 216 kwenye mechi 461.

MILAN, ITALIA

Comments are closed.