The House of Favourite Newspapers

Mimba ya Mapacha Yamsumbua Beyonce

Beyonce Knowles

STAA wa muziki, Beyonce Knowles kila mtu anajua alivyobeba mapacha tumboni kwake kwa sasa baada ya kutangaza na kuonesha tumbo live lakini ujauzito huo umeonekana kumsumbua kuliko ujauzito wa mwanaye wa kwanza, Blue Ivy.

Mtu wa karibu na familia hiyo ameuambia mtandao mmoja kuwa, Beyonce amekuwa akisumbuliwa na ujauzito huo hasa nyakati zasubuhi ambapo hupata kizunguzungu, usingizi, pamoja na kichefuchefu cha mara kwa mara na ikifi ka usiku kichwa humuuma sana.

Beyonce Knowles

Sosi huyo alisema: “Pamoja na matatizo hayo anayoyapitia lakini ni mwanamke anayejikaza na sapoti kubwa anaipata kwa mumewe (Jay Z) ambaye huwa naye karibu wakati wote hasa kwa kumnunulia maua, chokuleti na kumpetipeti kwani ana hamu ya kupata mapacha hao.”

Comments are closed.