The House of Favourite Newspapers

Idris Sultan Aganda Kifuani kwa Uwoya, Watu Waguna

Idris Sultan

Na MUSSA MATEJA| GAZETI LA IJUMAA| STAR MIX

MTANGAZAJI wa Choice FM ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Bongo, Idris Sultan amewashangaza watu  baada ya kufosi kumkumbatia msanii wa filamu Bongo, Irene Uwoya na hata alipokubaliwa, akaganda kifuani kwa mdada huyo kwa muda mrefu, hali iliyoibua miguno.

Irene Uwoya

Wawili hao walikutana kwenye shoo iliyopewa jina la LML iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita pale Leaders Club, Kinondoni jijini Dar ambapo baada ya Idris kumuona Uwoya, alimsogelea na ‘kumpliz’ amkumbatie.

Katika hali ya kushangaza, jamaa huyo alitulia kifuani kwa Uwoya kwa muda mrefu huku akimnong’oneza maneno ambayo hayakuweza kujulikana. Hata baada ya kuachiana, Idris alionekana kama aliyekuwa akitaka kulazimisha kukaa pembeni ya Uwoya lakini ikashindikana baada ya kuambiwa, kwenye kiti cha pembeni palikuwa na mtu.

Alipoulizwa ilikuwaje akamganda mrembo huyo, Idris alisema; “Hakuna la zaidi bwana, ni mambo ya kawaida kabisa, si unajua mimi na Uwoya tukoje

Comments are closed.