The House of Favourite Newspapers

Mimba yataka kumtoa roho Ester Kiama

MIMBA aliyo­nayo staa wa filamu za Kibongo, Ester Kiama ilitaka kumtoa roho baada ya kumsababishia kuumwa takribani miezi miwili bila kuinuka kitan­dani ambapo anadai alihisi kuchungulia kaburi kutokana na maumivu aliyokuwa nayo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda Es­ter alifunguka kuwa aliumwa sana mpaka akawa anaogopa hata kujionyesha kwa watu kutokana na alivyokonda kwani ujauzito alionao ulimsababishia kuwa na hali mbaya ingawa kwa sasa an­amshukuru Mungu anaendelea vizuri.

 

“Jamani nilichun­gulia kaburi kabisa, niliumwa sana lakini nafikiri ni kipindi tu cha mpito na niseme tu namshukuru Mungu kwa ku­nijaalia zawadi hii na ninamuomba sana anikamilishie safari yangu nimal­ize salama” alisema Ester Kiama.

Comments are closed.