The House of Favourite Newspapers

Mimi Mars; Ndugu, marafiki walimuogopa kwa umbeya

MSANII anayeku­ja kwa kasi katika gemu la muziki Bongo, Mariane Mdee ‘Mimi Mars’ amefun­guka kwamba enzi za utoto wake alikuwa na tabia ya umbeya, hali iliyosababisha ndugu zake akiwemo dada yake Vanessa Mdee ‘Vee Money’ kumkwepa.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Mimi Mars ambaye kwa sasa ana­tamba na kibao chake cha Kodoo alisema zamani alikuwa na tabia ya kuongeaongea hovyo kiasi cha kuwakera wen­gi lakini anashukuru Mungu alivyokua hiyo tabia akaachana nayo.

 

“Kweli ukiwa na utoto unakuwa na mambo mengi lakini ukikua unaacha, tabia yangu ya uropokaji na um­beya vilinifanya niogopwe. Yaani nikiwa nimekaa sehemu watu wananik­wepa lakini najua ilikuwa utoto tu, sasa nimekuwa nimeacha,” alisema Mimi Mars.

 

Mimi Mars alidai kuwa kitendo hicho kilikuwa kinamkera sana Vanes­sa na baadhi ya ndugu zake ambao ilifikia kipindi wakiwa wanaon­gea mambo yao wanam­fukuza kwani walikuwa wanajua atakachofanya.

Stori: Memorise Richard.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.