Minaj Aongelea Bifu na Remy Ma, Albamu Yake Mpya

rapper Nick Minaj

BAADA ya kusubiri kwa miaka mitatu, rapper Nick Minaj ametangaza ujio wa albam yake mpya. Msanii huyo albam yake ya mwisho ilitoka mwaka 2014 kwa jina la The Pinkprint ambayo ilifanya vizuri kutokana na baadhi ya nyimbo zake alizobeba tuzo mbalimbali.

rapper Nick Minaj

Hata hivyo, msanii Nick Minaj ameweka wazi jambo hilo wakati akiwa kwenye tamasha moja huko jijini New York akisema anawapenda mashabiki zake na wakae tayari kwa albam yake mpya ambayo itakuwa ni nzuri kuliko albam zote zilizotoka kwa wasanii wengine. Akaongoeza kwamba kwa hiyo, mashabiki wakae mkao wa kula kwa huo ujio wa albam yake, hiyo ikiwa mara ya kwanza kwa Nick Minaj kuweka wazi kuwa anatarajia kutoa albam yake.

Aliongeza kwamba anatambua itakuwa kati ya albam bora kuwahi kuzifanya kwa kuwa kila wakati huwa anaenda na muda na kwa sasa anafahamu ni kitu gani mashabiki zake wanataka.

Wakati huohuo, Nick Minaj alipoulizwa kuhusu bifu lake na Remy Ma alifunguka kuwa: ”Sikuanza kurap kwa ajili ya kushindana na mtu ila ninachotaka kusema ni kuwa nawashukuru mashabiki wangu kwa kuwa na mimi wakati wote na albam yangu mpya itakuwa kama zawadi kwao.”

Na : SAMSON JEREMIAH

Breaking News: Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa -Dar


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment