The House of Favourite Newspapers

Misri, Zimbabwe watatupa taswira ya Afcon

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jana Alhamisi ilikuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Misri ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).

 

Taifa Stars ambayo imepiga kambi nchini Misri tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kucheza na Misri, jana, baada ya hapo keshokutwa Jumapili itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe.

 

Katika michuano hiyo ambayo itafanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19, mwaka huu, Taifa Stars imepangwa Kundi C na timu za Kenya, Senegal na Algeria.

 

Kupata mechi hizo mbili za kirafiki ni hatua nzuri kulingana na kundi ambalo tupo. Misri na Zimbabwe ni kipimo tosha kwa Taifa Stars kuelekea Afcon.

 

Ukiangalia tunacheza na timu zote ambazo zipo Kundi A kwenye michuano hiyo huku moja ikiwa ni mwenyeji wa michuano. Lakini pia, kwa ubora wa viwango vya soka duniani, Misri imeiacha mbali Tanzania, lakini pia hata Zimbabwe nayo imetuacha nyuma.

 

Hivyo tutaipima vizuri timu yetu. Baada ya mechi hizo, Watanzania tutapata taswira halisi ya ubora wa timu yetu
hiyo na nini itafanya katika michuano hiyo tunayoshiriki kwa mara ya pili.

 

Hivi sasa baadhi ya Watanzania washaanza kuiona Taifa Stars haiwezi kufanya vizuri Afcon, ni mapema kusema hivyo. Tuwe wazalendo, tuisapoti kwa namna yoyote ile timu yetu.

Comments are closed.