The House of Favourite Newspapers

Miss Kachumbari wa Kachumbari Show apatikana

1Mshindi wa Miss Kachumbari, Anna Mbawala akiwa amepozi baada ya kuibuka mshindi.

2

…Akiwa na warembo wengine.

3Msanii chipukizi wa Bongo Fleva akitumbuiza kwenye tamasha hilo.

4Maigizo yakiendelea kutawala kwa mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo

5Maigizo yakiendelea jukwaani.

6Baadhi ya mashabiki wakipiga picha katika ‘red carpet’ iliyokuwa imeandaliwa.

7Upigaji picha ukiendelea.

8Mashabiki wakiendelea na picha.

9Baadhi ya mashabiki wakifuatilia vichekesho vilivyokuwa vikiendelea.

10Kikundi chipukizi cha maigizo kikionyesha uwezo wake kwa mashabiki waliofika kwenye shoo hiyo.

Na Denis Mtima/Gpl

JANA (Jumamosi) katika Ufukwe wa Coco jijini Dar lilifanyika tamasha lililopewa jina la Kachumbari Show ambapo pia alipatikana Miss Kachumbari aitwaye Anna Mbawala aliyeshinda kupitia kura zilizopigwa na watumiaji wa Mitandao ya Whatsapp na Instagram kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Tamasha hilo liliandaliwa na Kampuni ya Timamu African Media chini ya Mkurugenzi wake, Timothy Conrad, ambapo zilipostiwa picha mbalimbali za warembo kupitia mitandao hiyo kisha wadau wakapiga kura kumchagua yule ambaye ni bomba zaidi na hivyo Anna akaibuka kidedea.

Akizungumzia lengo la tamasha hilo litakalokuwa linafanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, Timothy alisema lengo ni kuibua warembo wanaoweza kupata fursa za kuwa mabalozi wa bidhaa au makampuni mbalimbali, kupata nafasi za uigizaji na pia kutafuta vijana chipukizi katika fani ya vichekeso (komedi).

Comments are closed.