MITIHANI YA ZAHERA MSIMU HUU USIPIME!

MIONGONI mwa makocha wenye mtihani mgumu msimu huu ni Mwinyi Zahera wa Yanga. Msimu uliopita ulimpitia salama kabisa na hakukuwa na yoyote aliyemnyooshea kidole ingawa alikuwa miongoni mwa makocha walalamishi sana.
Alikuwa akilalamikia marefa pamoja na mamlaka za usimamizi wa ligi kwamba mambo mengi yalikuwa hayaendi sawa na timu yake ilikuwa inaminywa.
Lakini vilevile Yanga hawakumlalamikia sana kutokana na mafanikio aliyoyapata na aina ya kikosi alichokuwanacho. Msimu huu kikombe kimeegemea upande wake. Hana cha kujitetea, amepewa kila kitu alichotaka na amekiri mwenyewe kwamba kikosi kilichosajiliwa ni chake.

Leo Jumapili anawasha mitambo rasmi kwenye Uwanja wa Taifa kwa kucheza dhidi ya Kariobang Shars ya Kenya. Mitihani ifuatayo inamuandama Kocha huyu anayependa kuvaa kaptula;
WACHEZAJI HURU Wakati anaanza usajili kuna mashabiki walikuwa wanajiuliza kwanini anasajili wachezaji wa kigeni ambao ni huru?
Mchezaji mzuri anawezaje kuwa huru? Lakini yeye akasisitiza kwamba anawajua vizuri na ni watu wa kazi. Uongozi ulimtetea kwamba hata hapo awali wachezaji wengi wa kigeni waliokuwa wanasajili nchini walikuwa huru ila kuna madalali waliokuwa wanawatumia kupiga mkwanja. Kama Wachezaji hao wasipomuangusha Zahera atakuwa ameshinda turufu nyingine ndani ya Yanga ambayo itamuongezea heshima nchini.

KIMATAIFA Ana mtihani wa kuhakikisha Yanga inaanza Ligi ya ndani ikiwa bado kwenye michuano ya kimataifa. Anashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu akiwa na Yanga na inaanza kabla ya Ligi haijaanza.
Ameonyesha umahiri mkubwa akiwa na Yanga kwenye Ligi ya ndani, mashabiki pia wameweka imani kubwa kwake na wanamtafsiri kama mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo. Heshima yake itaingia madoa kama ataondoshwa mapema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na mtani wake Simba akaendelea. Ana kazi ya ziada ya
MITIHANI YAZA HERA
kutumia kikosi kipya alichokiunda kulinda heshima yake na vilevile kuirejesha Yanga ubora wake kimataifa. Kipimo chake cha kwanza ni kuhakisha timu hiyo inafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini akiteleza kidogo haswa kwenye mechi mbili za awali dhidi ya Township Rollers ya Botswana anaweza kujikuta nje ya mashindano kabla hata msimu mpya wa Ligi Kuu Bara haujaanza.

LIGI YA NDANI
Yanga kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara siyo ishu, wanayo makombe kibao kabatini pale Jangwani lakini siyo ya Zahera. Hakuna lugha yoyote anayoweza kutumia Zahera kuwashawishi Yanga kwamba yeye ni Kocha mzuri kama wasipoona Kombe pale Jangwani. Tena mbaya zaidi lirudi tena
Simba,watamng’oa. Kikosi alichosajili msimu huu kitakuwa na ushindani mkubwa na kitaongeza utamu kwenye Kombe la FA na Ligi.
Uongozi wa Yanga umesisitiza kwamba msimu huu wana kila sababu ya kubeba ubingwa kutokana na aina ya usajili waliofanya.
WANANCHI NA SIMBA Mashabiki na wanachama wa Yanga msimu huu wako karibu na timu hiyo kuliko misimu yote iliyopita.
Hiyo inatokana na michango yao waliotoa ya fedha kwa njia mbalimbali ili kuchangia gharama za uendeshaji wa timu pamoja na usajili hivyo macho yao yote yatakuwa kwa Zahera na kikosi chake. Lakini hata kivuli cha Simba kitakuwa na changamoto kubwa kwa Zahera.
Ushindani mkubwa ulioanzia kuanzia kwenye usajili mpaka leo kwenye Wiki ya Mwananchi utaendelea mpaka Uwanjani. Yanga hawatakuwa na tabasamu kwa Zahera kama Simba itamzidi kwa mafanikio ndani na nje.


Comments are closed.