The House of Favourite Newspapers

WACHEZAJI WA YANGA WATASEPA NA KIJIJI TAIFA LEO

PAMOJA uzi mpya, kumisi mechi za Yanga lakini wadau wengine wanakwenda Taifa leo kwa kazi moja tu. Kuona kikosi kipya kinafananaje? Yale waliokuwa wakiyasoma kwenye magazeti ni kweli yamo? Mechi ya Yanga na Kariobang Sharks ndiyo itakayoonyesha uhalisia. Mastaa hawa ndio watakaotazamwa zaidi leo kwenye Uwanja wa Taifa;

 

DAVID MOLINGA Huenda ndiye mchezaji ambaye mashabiki walikuwa wanaomba pakuche waingie Taifa kumuona akiwa kwenye jezi ya Yanga na jinsi.

DR Congo wanamuita Falcao na alisajili dakika za mwisho na Mwinyi Zahera. Ni mchezaji ambaye Zahera amewaaminisha mashabiki kwamba ni bonge la straika hata Heritier Makambo anasubiri. Falcao ni kipande cha mtu.

PATRICK SIBOMANA Atakachokifanya Taifa leo huenda kikamjengea jina na kupiga mhuri wa moto kwenye nyoyo za mashabiki wa Yanga. Mashabiki wanatumia sana jina lake mitaani kutamba. Kwenye mechi za kirafi ki huko Morogoro katupia hat trick na kupiga vyenga vya kutosha. Simba wakabeza kwamba ilikuwa ni mechi laini, lakini yeye aliwajibu kwamba ameiva na ataonyesha ubora wake Taifa.

ISSA BIGIRIMANA Wanamuita Walcott akifananishwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa yupo Everton,Theo Walcott. Kikubwa ni mbio alizonazo na umahiri wake. Akiwa huko Morogoro tayari aliwaonyesha mashabiki mazoezini kwamba ana kitu cha ziada, lakini kwenye nyasi za Taifa leo huenda burudani yake ikawa mara mbili huku akionekana kupania sana.

 

JUMA BALINYA Ndio mchezaji wa kwanza mpya mwenye jina kubwa kutoka nje ya nchi kutambulishwa Yanga. Alitokea Polisi ya Uganda huko alikuwa mfungaji bora katika ligi ya nchi hiyo baada ya kuifunga mabao 19, hilo linawachanganya sana mashabiki wa Yanga kwani wanataka kufahamu ubora wake. Lakini pia huko Morogoro kwenye mechi za kirafi ki hakupoa kabisa, alitupia na kutoa asisti kadhaa.

SADNEY URIKHOB Ni Mnamibia ambaye ameapa kuja kufanya kweli
na huyu ndiye atachukua nafasi yake kikosini. Beki huyo mwenye umri wa kati anakumbukwa wakati alipokuja kufanya majaribio katika timu ya Simba,lakini kwa wapenzi wa Yanga hawamfahamu vyema.

 

MUSTAPHA SULEIMAN Yanga ilimsajili beki huyo kisiki kutoka Burundi ili kuimarisha ulinzi akishirikiana na Kelvin Yondani. Akiwa na klabu ya Aigle Noir ya Burundi msimu uliopita
alionyesha utofauti ambao Yanga wanataka kuona leo Taifa.

FAROUK SHIKALO Hakuna haja ya kutafuna maneno. Ndiye kipa namba moja wa Yanga msimu huu. Huyu Mkenya ndiye aliyebariki safari ya bwana Klaus Kindoki kurudi DR Congo kuangalia utaratibu mwingine wa
kupata riziki. Farouk ni kipa namba moja wa Kenya
na amekuwa mahiri sana katika siku za hivi karibuni akiichezea Bandari ya Mombasa.

 

ISSA MWARAMI MARCELO Kaja kwa kazi maalumu ya kuziba pengo la Gadiel Michael ambaye ni mali ya Simba kwa sasa,ni jina jipya kabisa ambalo mashabiki

Comments are closed.