Miwani za Mastaa Zilizotikisa Msiba wa Masogange!

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Harmonize

UNAPOMUONA mtu amevaa miwani, awe mwanamke au mwanaume, mtoto au mtu mzima ujue huyo ana matatizo ya macho au kavaa kwa ajili ya fasheni tu.

Ali Saleh Kiba ‘Alikiba

 

Hata hivyo, asilimia kubwa ya wanaovaa miwani, hasa kwa upande wa mastaa wengi wao ni kwa fasheni tu na ndiyo maana miwani zipo zilizodizainiwa kikatuni na nakshinakshi kibao, nyingine kubwa kiasi cha kuweza kuwa gumzo endapo mtu ataivaa.

 

 

Hili limethibitishwa na kile kilichoonekana kwenye msiba wa Agness Gerald Waya ‘Masogange’ aliyefariki hivi karibuni.

Kwa waliofuatilia zoezi la kuagwa kwake pale Leaders Club, Kinondoni jijini Dar watakuwa wameshuhudia mastaa kibao ambao walitinga wakiwa wamevaa miwani za jua na nyingine za kawaida tu ikiwa ni katika hali ya kutaka kuficha macho yao, aidha ili wasio-nekane pale wataka-pokuwa wanatokwa na machozi au aibu.

Orodha ya mastaa waliotinga urembo huo ni ndefu lakini hapa nitakupa 10 waliotikisa ambao ni Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Husna Maulid, Nice Chande, Aunt Ezekiel, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Jacqueline Wolper na Rose Ndauka

Risasi Vibes


Loading...

Toa comment