The House of Favourite Newspapers

MJADALA HOT; UNA LIPI JUU YA RIPOTI YA JANA YA CAG?

Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini, (CAG) Professa Musa Juma Assad, jana alitoa ripoti yake kuhusu hesabu za mashirika ya umma na idara za Serikali.

Mwaka 2016 CAG Assad alitoa ripoti yake na ilimpa hasira Rais Dk John Magufuli, akamsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk Ally Simba.

 

Rais alimsimamisha kazi Dk Simba kutokana na kile alichodai kushindwa kusimamia ipasavyo mkataba wa utekelezaji wa mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS), kitendo kilichosababisha nchi kukosa mapato ya Sh bilioni 400 kwa mwaka – zaidi ya Sh trilioni 1 kwa kipindi cha miaka mitatu tangu walipoingia mkataba na Kampuni ya SGS Machi 22, 2013.

 

Jana makampuni zaidi ya 11 yamebainika na CAG kuendeshwa kwa hasara na Polisi kuteketeza mabilioni ya fedha. Nini maoni yako kuhusu hili? Na unadhani Rais JPM atafanya nini?

Changia, lakini bila kutoa tusi.

Comments are closed.