The House of Favourite Newspapers

JPM Awaweka Mtu Kati, Mkurugnzi & Mhandisi Njombe – VIDEO

Rais Dkt John Magufuli amewaweka mtu kati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Njombe na Mhandisi wa halmashauri hiyo kutokana na mradi mbovu wa maji katika eneo la Manga tangu mwaka 2009 hadi sasa huku akimtaka Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa kuhakikisha mradi huo unatoa maji.

 

Magufuli amefanya hay, wakati akihutubia maelfu wa wananchi uwanja wa Polisi Makambako leo Alhamisi Aprili 11, 2019 ambapo amefungua barabara ya Mafinga-Nyigo-Igawa yenye urefu wa kilomita 138.7 katika eneo la Mtewele, baada ya malalamiko ya mmoja wa wananchi wa eneo hilo aliyekuwa amebeba bango lenye kero hiyo ya maji alipokatazwa kuliwasilisha ndipo Rais akamuita jukwaani ili aseme kero yake iweze kutatulia.

 

“Wananchi wa hapa tuna shida ya maji, tuna miezi zaidi ya sita hatujapata maji, lakini ulipokuja wewe mheshimia rais wameleta maji, tumekuwa tukiteseka, tangu mwaka 2009, mradi umekamilika lakini hautoi maji,” alisma kijana huyo.

 

Rais Magufuli alitoa maagizo kwa Waziri Mbarawa kubaki Njombe na kuhakikisha tatizo hilo la maji analishughulilia haraka.

 

“Yale yote yaliyozungumzwa na mbunge na wananchi ninaahidi kuwa tutayafuatilia na ninataka maeneo yote ya Makambako ambayo hayajapata umeme yapate, wakati mwingine nikienda kwenye mikutano watu wanazuiwa kuonesha mabango yao, hii nchi ni yenu na mimi ni rais wenu hivyo onyesheni mabango yenu ili nijue matatizo yenu.

 

“Viongozi wote niliowapanga hapa na wa kitaifa kwa ujumla mnatakiwa mtatue changamoto zote wanazozipata wananchi kwaajili ya maendeleo ya nchi, nawapeni Pongezi sana wananjombe kwakua mkoa pekee ambao hauna Nyumba za Nyasi hakika ni mkoa ambao wengi wanapaswa kujifunza kwenu,” amesema Magufuli.

TAZAMA ALIVYOWAKAANGA VIGOGO HAO

Comments are closed.