The House of Favourite Newspapers

MJANE TANGA ALIYEMLILIA JPM MAPYA TENA

MAPYA tena yameibuka kwa yule mwanamke aliyejitokeza mbele ya Rais Dk. John Magufuli kudai amethulumiwa mali na baadaye kufungwa miezi mitatu kwa kosa la kuingia kwa jinai eneo la bomba la mafuta, Swahiba Shosi kwani amepata Wakili Obediodom Chanjarika wa kumtetea na tayari amekata rufaa kupinga adhabu hiyo akibainisha mambo mawili.

 

Swahiba alijipatia umaarufu baada ya kuangua kilio mbele ya Rais Magufuli wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria Februari 2 mwaka jana jijini Dar es Salaam . Mwanamke huyo tayari anatumikia kifungo chake katika Gereza la Maweni lililopo nje kidogo ya Jiji la Tanga lakini Wakili Chanjarika aliwasilisha rufaa ya mama huyo mwishoni mwa wiki iliyopita kwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Hilda Lyatuu na ilitarajiwa kusikilizwa jana Jumatatu.Wakili Chanjarika ameomba maombi mawili, moja, ameomba rufaa kupinga hukumu iliyompeleka chaguo la kulipa faini, jela au kifungo cha nje.

 

Pia anadai kuwa hakukuwa na ushahidi wowote kuonyesha mmiliki wa eneo hilo na hati ya mashitaka ina upungufu kutokana na kutoonyesha kifungu ambacho kilitumika kumtia mteja wake gerezani na pili amemuombea dhamana ya kuwa nje wakati akisubiri kusikilizwa kwa rufaa yake.

 

Kwa mujibu wa rufaa hiyo, wakili wa mama Swabaha anadai kuwa hukumu hiyo ilikuwa na upungufu kisheria kwa sababu haikuwa na  Tayari Hakimu Lyatuu amemuagiza Wakili wa Serikali, Rebeca Msalangi kuwakilisha hati kinzani ya kiapo ili aanze kusikiliza shauri hilo na jana hakimu huyo alitarajia kusikiliza hoja hizo na za upande wa serikali.

STORI: NA MWANDISHI WETU, TANGA

Comments are closed.