Mjane wa Kobe Bryant Alipwa Dola Milioni 16 baada Picha za Mumewe Kuvujishwa
BAADA ya picha za mwili wa aliyekua nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani Kobe Bryant kuvujishwa na naibu afisa wa polisi ambaye alisambaza picha hizo kwenye mitandao. Hivyo mahakama imeamuru Mke wa marehemu Kobe alipwe dola milioni 16 kama fidia kutokana na kuvuja kwa picha hizo.
Mke wa wa Kobe Bi Bryant alitoa ushahidi huku akibubujikwa na machozi wakati wa kesi hiyo katika siku 11 alisema kwamba habari za picha hizo zilizidisha huzuni yake baada ya kumpoteza mumewe na bintiye kwenye ajali hiyo iliyotokea 2020.
Alipokua akishuhudia kuhusu tukio hilo amesema tukio hilo limemfedhehesha sana na kumfanya aingiwe na uoga,picha hizo zilionyesha mwili wa marehemu kobe.
“Nilihisi kutaka kukimbia na kwenda kujitupa kwenye maji na kupiga kelele, tatizo siwezi kukataa uhalisia wangu siwezi kuukimbia mwili wangu” alisema Bi Bryant
Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa Mitandao