The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mkude: Kwa muziki wa Shiboub kazi ipo

KIKOSI cha Simba kimerejea nchini juzi Jumatano kikitokea Afrika Kusini kilipokuwa kimeweka kambi yake ya wiki tatu ya kujiandaa na na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara lakini pia michuano ya kimataifa.

 

Hata hivyo, kiungo mkabaji wa timu hiyo ambaye pia amewahi kuwa kiungo bora mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya Sudan, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman aliyesajiliwa na Simba hivi karibuni amemwagiwa sifa kibao na kiungo mkongwe kikosini hapo, Jonas Mkude.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mkude ambaye sasa yupo na kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa na mchezo wa kimataifa wa marudiano dhidi ya Kenya, amesema kuwa anavutiwa sana na aina ya uchezaji wa kiungo huyo ambaye Simba imemsajili akitokea Al Hilal ya Sudan.

 

Alisema kuwa Shiboub ni moto wa kuotea mbali kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo mkabaji na kuongeza asipokuwa makini anaweza kupoteza nafasi katika kikosi hicho.

 

“Kusema kweli kwa huyu jamaa ninatakiwa nijipange kwelikweli kwani anajua, naupongeza uongozi kwa usajili wake.

 

“Lakini pia kwa jinsi alivyo hata pengo la James Kotei naamini halitakuwepo kutokana na ubora wake,” alisema Mkude na kuwataka wapenzi na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani katika tamasha la Simba Day ili waje kuwaona wachezaji wapya waliosajiliwa akiwemo Shiboub watakapokuwa wakipambana na Power Dynamos ya nchini Zambia

Comments are closed.