The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi Mtendaji Tigo Aungana na ‘DREAM TEAM’ Kuhudumia Wateja

0
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Mwangaza Matotola akizungumza kwenye hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji, Simon Karikari.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Simon Karikari, leo ameingia mtamboni na watoa huduma wake aliowaita ‘Dream Team’  na kuwahudumia wateja katika kitengo cha kupokea simu za kusikiliza shida za wateja wao.

Karikari alifanya hayo kwenye hafla ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika kituo chao cha mawasiliano na wateja wao kilichopo Morocco Dar.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Tigo, David Umor akiwapongeza watoa huduma wa kampuni hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Kabla kuanza kutoa huduma hizo Karikari alianza kuzungumza na watoa huduma wa kituo hicho kwa kuwasalimia kwa kauli mbiu yao ya mwaka huu ambayo ni ‘Dream Team’ .

Baada ya salamu hiyo aliwapongeza watoa huduma hao kwa kazi kubwa wanayofanya mpaka kujiita Dream Team kutokana na umahiri wa kazi yao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari (katikati mwenye koti la kijivu) akiwaongoza maofisa wa kampuni hiyo kukata keki kwenye hafla hiyo.
Sehemu ya watoa huduma hao wakishuhudia mambo yanavyoendelea.

“Kwanza niwapongeze sana kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya hali inayopelekea tuzidi kuongoza kila kukicha.

“Najua mnafanya kazi ngumu na yenye changamoto nyingi lakini mmeweza kuikabili vizuri na kufanya tuzidi kusonga kwa hilo hongereni sana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari akiwa mtamboni kupokea simu zilizokuwa zikipigwa na wateja wenye changamoto mbalimbali.

“Napenda kuwashukuru kwa utendaji wenu mzuri na mungu awabariki mzidi kuchapakazi zaidi ahsateni na endeleeni kuwahudumia wateja wetu”. Alisema mkurugenzi huyo.

Baada ya kusema hayo mkurugenzi huyo alianza kutoa huduma kwa kupokea simu zilizokuwa zikipigwa na wateja waliokumbana na changamoto huko walipo na kuwatatulia changamoto zao.

Kampuni ya Tigo imeendelea kufanyakazi kiukaribu na wateja wao huku ikiwashukuru kwa kuwa nao kipindi chote tangu kampuni hiyo ianze kutoa huduma zake hapa nchini.               HABARI/PICHA:RICHARD BUKOS

Leave A Reply