The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi WHO Aambukizwa Corona

0
        Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus.

 

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, amelazimika kujitenga kwa siku 14 baada ya mtu mmoja aliyepatikana na COVID-19  kumtaja kama mmoja wa watu wa karibu aliokutana nao hivi karibuni.

 

Amesema, “Nimetajwa kama mmoja wa watu waliokutana na mtu aliyepatikana na ugonjwa huo, nipo vizuri na sina dalili lakini nitajiweka karantini kwa siku zijazo, kwa mujibu wa taratibu za WHO, nikifanya kazi kutokea nyumbani.”

 

Ameongeza kuwa ni muhimu kwa watu wote kufuata taratibu za kiafya zinazotolewa kwani kufanya hivyo kutavunja mnyororo wa maambukizi ya COVID-19, kuvizidi nguvu na kulinda mifumo ya afya

 

Kauli yake inakuja wakati mataifa barani Ulaya — Switzerland na Uingereza  — yakiingia katika awamu mpya ya ‘lockdown’ kufuatia ongezeko la maambukizi.

Leave A Reply