The House of Favourite Newspapers

Mkutano wa Dharura wa Yanga Waota Mbawa

MKUTANO wa dharura wa Yanga uliokuwa ufanyike leo Jumamosi, umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena hapo baadaye.

Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam kabla ya kusogezwa mbele.

 

Mkutano huo uliitishwa na Kamati ya Utendaji ya Yanga iliyokutana hivi karibuni na kukubaliana kufanya mkutano huo, kabla ya kwenda kwenye uchaguzi wa klabu hiyo uliopangwa ufanyike Januari 13, mwakani.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, mkutano huo hautafanyika huku leo wakipanga kufanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea sababu za kusitisha mkutano huo.

Mtoa taarifa huyo alisema, katika mkutano huo walipanga kujadili ajenda mbili muhimu ambazo ni uchaguzi wao mkuu na mustakabali wa msimu huu na ujao wa Ligi Kuu Bara.

 

“Kama unavyofahamu uchaguzi wetu unafanyika mwakani, hivyo tulipanga ni lazima tukutane wanachama wote kwa ajili ya kuzungumza mambo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi wetu.

 

“Katika mkutano huo, mwenyekiti wetu Yusuf Manji alitarajiwa kuwepo na kikubwa kuthibitisha kuwa yupo kwenye timu,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Usajili na Mashindano wa Yanga, Hussein Nyika alithibitisha hilo la kusitishwa kwa mkutano huo wa leo.

“Mkutano hautakuwepo kama tulivyopanga awali na sababu tumepangaza kuzitaja kesho (leo) baada ya kufanya mkutano na Waandishi wa Habari,” alisema Nyika.

Stori na Wilbert Molandi na Sweetbert Lukonge | Championi Jumamosi

HARMONIZE alivyompigia WOLPER magoti Stejini, MAUNO Kama yoteee!!

Comments are closed.