The House of Favourite Newspapers

Mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM Zanzibar D.k Shein

0

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi na Wana CCM katika mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mpira Bungu Wilaya ya Kati Unguja na kuomba Kura kuendelea kuiongoza Zanzibar kwa Maendeleo katika sekta mbalimbali za Kijamii na kuendeleza kukuza Uchumi wa Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai akiwahutubia WanaCCM wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM akisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambayo ilivyotekelezwa kwa kiasi kikubwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar, na kuwataka Wananchi kumchagua Dk Shein kwa maendeleo zaidi kwa Zanzibar na Wananchi wake.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia Wananchi wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya mpira Bungi Wilaya ya Kati Unguja.

Kada wa CCM Bi Amina Salum Ali akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM na kuwata kumpigia Kura ya Ndio Dk Ali Mohamed Shein, ili kuendelea kuwaletea maendeleo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla akiwahutubia Wananchi wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika viwanja vya mpira Bungi Unguja.

Wanachama wa CCM wakiingia katika viwanja vya mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakiwa na picha za Wagombea.

Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla alipowasili katika viwanja vya Bungu kuendelea na Kampeni zake za kugombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM.

Mgombea Urais wa Zanzibar pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya bungi kuaza kwa kampeni yake akiwa na Viongozi wa CCM kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai na kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla, wakielekea jukwaa kuu kwa ajili ya mkutano huo.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika viwanja vya mpira bungu kuhudhuria Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Dk Ali Mohamed Shein. uliofanyika katika viwanja vya bungi.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangia wakati wa Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM uliofanyika katika viwanja vya Bungi Wilaya ya Kati Unguja.

Wanachama wa CCM wakimshangilia Mgombea wa Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein wakati akiwahutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vha mpira Bungi Wilaya ya Kati Unguja.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, wakati akihutubiwa Wananchi katika Mkutano wake wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya mpira Bungi Unguja.

Leave A Reply