The House of Favourite Newspapers

MKUU WA KAMPUNI YA ACACIA ASHTAKIWA

Image result for asa mwaipopo acacia
Asa Mwaipopo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchimbaji madini Tanzania Acacia Mining, Asa Mwaipopo,  amefikishwa mahakamani hii leo kwa mashtaka ya uhalifu wa kiuchumi.

Mwaipopo mwenye umri wa miaka 55 alikamatwa  jana mjini Dar es Salaam na anajiunga na wengine sita ambao wanashikiliwa tangu wiki iliyopita kwa makosa kama ayo akiwemo Deogratias Mwanyika aliyekuwa makamu wa rais wa kampuni ya Barrick Gold na mkurugenzi wa mawasiliano wa kampuni ya Bulyanhulu Mine, na Alex lugendo mwenye umri wa miaka 41 ambao tayari wako rumande.

Mwaipopo alifikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu jana ambapo alishtakiwa kwa kupanga njama na maofisa wengine ndani na nje ya Tanzania na kughushi nyaraka kukwepa kulipa kodi. Acacia imekuwa katika mgogoro na serikali ya Tanzania, tangu serikali izuie usafirishwaji wa makinikia ya kampuni hiyo nje ya nchi.

Serikali pia imekuwa ikiishutumu kampuni ya Acacia kwa kukwepa kulipa kodi inayostahili, tuhuma ambazo kampuni hiyo mpaka sasa imekuwa ikizikanusha.

Image result for asa mwaipopo acacia

Acacia inasema nini:

Kwa mujibu wa shirikala habari la Reuters, Acacia Mining ilithibitisha siku ya Jumatano wiki iliyopita kwamba mfanyakazi wao na aliyekuwa mfanyakazi wa kampuni hiyo, walikamatwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) ikiwa ni wiki moja baada ya kampuni hiyo kusema mfanyakazi mwingine ameachiwa kwa dhamana baada ya kushtakiwa kwa rushwa.

Kampuni hiyo inamilikiwa na kampuni ya nchini Canada iitwayo Canada Barrick Gold.

Acacia mining

Mvutano wa Acacia Mining na serikali ya Tanzania?

Serikali ya Tanzania imeishutumu Acacia kwa kufanya kazi ya uchimbaji nchini Tanzania kinyume cha sheria na kusema kuwa makampuni ya uchimbaji madini yamekuwa yakikwepa kulipa kodi. Kutokana na tuhuma hizo kutoka kwa serikali ya Tanzania, thamani ya hisa za kampuni ya Acacia ilishuka. Uchunguzi ulioamriwa kufanyika mwezi Machi mwaka jana ulibaini kuwa Kampuni ya uchimbaji Acacia imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.

Mwenyekiti wa kamati ya wachumi na wanasheria Nehemiah Osoro iliyofanya uchunguzi huo alieleza. Kamati ilifanya uchunguzi kuhusu usafirishaji wa madini kwa kipindi cha miaka 19. Hisa za Kampuni ya Acacia ambayo inamilikiwa na Barrick Gold Corporation zilianguka kwa kiasi cha asilimia 15. Acacia imejitetea kuwa inafanya biashara zake kwa viwango vya juu na inafanya kazi kwa kufuata sheria za Tanzania ikiwemo kulipa kodi zote.

Comments are closed.