The House of Favourite Newspapers

Juventus Yaipiga Man U Nyumbani, Matokeo Yote Uefa Haya Hapa

MANCHESTER United wameangukia pua katika Uwanja wao wa Old Trafford kwa kukubali kichapo cha goli moja bila kutoka kwa timu ya Juventus wa Italia.

Nyota mpya wa Juventus ambaye amewahi kukIpiga na United hapo awali, Cristiano Ronaldo, aligeuka mwiba mchungu kwa mashabiki wake wa zamani   usiku wa kuamkia leo.

Krosi ya Ronaldo ndiyo ilizaa goli lilofungwa na Paulo Dybala katika dakika ya 17 ya kipindi cha kwanza.

Mashetani Wekundu  hao waliamka kiasi mwanzoni mwa kipindi cha pili na kufanya shambulizi la maana kupitia kiungo Paul Pogba lakini shuti lake liligonga mwamba.

Usiku wa jana ulikuwa mgumu kwa kocha wa Manchester United, Jose Mourinho, ambaye alifanyiwa kebehi na mashabiki wa Juve.

Kipigo cha jana kilikuwa cha pili kwenye mashindano ya Ulaya toka mwaka 2013 kwa Manchester United wakiwa nyumbani Old Trafford.

Mwaka 2013 United walifungwa na Real Madrid na Ronaldo alipachika bao la ushindi.

Juve na United watacheza mechi ya marudio katika Uwanja wa Allianz  Novemba 7, 2017.

Iwapo Juve yenye alama 9 na inayoshika usukani wa Kundi H itashinda mchezo huo itafuzu katika hatua ya mtoano (16 bora).

United wanasalia katika nafasi ya pili na alama zao 4. Valencia wana alama 2 na Young Boys wanashikilia mkia wakiwa na alama 1.

Jose Mourinho

Bodi ya Manchester United bado inamkubali Jose Mourinho

Mourinho amekubali kushindwa akisema Juve walikuwa na kiwango bora Zaidi. “…Juventus wapo katika kiwango cha tofauti nasi. Yanipasa kuwa muwazi. Ubora, ukomavu na uzoefu wao ni wa kiwango cha juu. Ilikuwa mechi ngumu sana kwetu. Nilifikiri tungeambulia kitu lakini haikuwezekana.”

MATOKEO YA MECHI ZOTE ZILIZOPIGWA USIKU WA KUAMKIA LEO

Comments are closed.