The House of Favourite Newspapers

Mkuu Wa Mkoa Wa Kilimanjaro, Anna Nghwira Ashiriki Tamasha La Kili Dome

0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Nghwila akizungumza na baadhi ya wakazi wa moshi na washiriki wa mbio za Kilimanjaro Marathon ambao ndio waandaaji na wadhamini wa tamasha hilo alipotembelea kushirikinao tamasha hilo kuelekea kilele cha mbio hizo 2020 zinazotarajiwa kufanika leo Mkoani humo.Tamasha hilo lilifanyika katika Bustani ya Hugo’s Moshi Kilimanjaro jana.Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Nyanda za juu Kaskazini, Jemes Bokella.

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro jana ameshiriki Tamasha kubwa la Kili Dome lililo andaliwa na Kampuni ya Bia Nchini(TBL) kuelekea kilele cha mbio za Kili Marathon zinazotarajiwa kufanyika leo Moshi Mkoani Kilimanjaro.

 

Akizungumza na baadhi ya washiriki wa mbio hizo na  wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa usalama wa Mkoa huo uko sawa sawa na wamejipanga vizuri kuhakikisha waliotoka mikoani na Nchi za nje wanaingia na kutoka salama wasiwe na wasiwasi na akawatakia mbio njema za Kili Marathon 2020 zenye Amani tele pamoja na makazi mema ya mji wa moshi kwa siku watakazokaa.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Nghwila na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania Kanda ya Nyanda za juu Kaskazini, Jemes Bokella wakicheza kuashilia ukaribisho maalumu waa mashindano ya Kili Marathon 2020 yanayotarajiwa kufanika leo Mkoani humo.Tamasha hilo lilifanyika katika Bustsni ya Hugo’s Moshi Kilimanjaro jana.

Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na mamia ya watu lilikuwa na burudani za kutosha za muziki wa dansi zilizofunguliwa na Mwanamuziki, Maua Sama, Makomando, G Nako, Marioo na Mimi Mars ambao walikonga nyoyo za waliohudhuria tamasha hilo kila mmoja kwa wakati wake.

Nae Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Iren Mutiganzi alimshukuru Mkuu wa Mkoa ambaye ameonyesha upendo wa pekee kwa Mashindano na kwa wageni wote waliokwenda kushiriki mashindano kwa kushiriki nao tamasha la usiku ambalo hukutanisha wadau na washiriki wote wa mbio za marathon lakini pia kuwahakikishia usalama wakati wote mpaka watakapoondoka mkoani hapo.

“Kilimanjaro Marathon inatarajiwa kufanyika leo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa kushirikicha wawakilishi kutoka katika nchi zaidi ya 52 hivyo ni sifa kwetu kama waandaaji watu wote wakaingia kwa Amani na kutoka kwa Amani kama alivyotuhakikishia usalama Mkuu wa Mkoa”, alimaliza kusema Mutiganzi.

Leave A Reply