The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Azuiwa Kuingia Mgodi wa Bulyanhulu

0

KAHAMA: Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellack umezuiwa kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini(TMAA).

Maofisa hao waliondoka mara baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu kupokelewa na Rais John Magufuli.

Akizungumza kwa njia ya simu jioni hii, Tellack anayefanya ziara ya kikazi wilayani Kahama amesema ameagiza jeshi la polisi kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.

Mapema leo, mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.

Katika mgodi wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.

Leave A Reply