The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Uchunguzi TAKUKURU Atoa Ushahidi Dhidi ya Kesi ya Gugai

0
Katika kizimba cha mahakama ya Kisutu ni aliyekuwa ni aliyekuwa Mhasibu Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Godfrey Gugai, George Makaranga,Leonard Aloys na Yasin Katera.

 

SHAHIDI ambaye ni Mkuu wa Uchunguzi na Usalama Katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Mtalai ameiambia mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kuwa yeye ndiye aliyeambiwa na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Kamishna, Valentino Mlowola kumpa ilani ya kujieleza mtuhumiwa Godfrey Gugai juu ya uhalali wa umiliki wa mali zake.

 

Ushahidi huo ameutoa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa, ambapo akimhoji shahidi alimuuliza kama endapo akioneshwa nyaraka za vielelezo vya umiliki wa mali alizoorodhesha mshatakiwa Gugai akama anaweza kuvitambua? Aliuliza swali.

 

Katika majibu yake shahidi amesema kuwa anaweza kuvitambua, amabapo wakili mbagwa amemuonesha na kukiri kuwa vielelezo hivyo nisahihi na anavitambua.

 

Katika katika swali aliloulizwa na wakili wa serikali lilielekeza juu ya matokea ya uchunguzi uliofanywa na timu ya TAKUKURU kuwa ulibani nini kutoka kwa mshtakiwa?

 

Shahidi akieleza juu ya swali hilo aliloulziwa na wakili Mbagwa amesema kuwa uchunguzi ulibaini yakuwa majibu yaliyotolewa na mshtakiwa Gugai hayakuwa sahihi kwa kuwa kulikosekana vielelezo vinavyoonesha mtuhumiwa kuhamisha umiliki wa baadhi ya mali alizokuwa akizimiliki.

 

katika kesi ya utakatishaji fedha, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake

 

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, makosa 19 kati ya hayo ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya Januari mwaka 2005 na Desemba mwaka 2015.

 

Inadaiwa mshitakiwa akiwa jijini Dar es Salaam kama mwajiriwa wa TAKUKURU alikuwa akimiliki mali za zaidi ya sh. bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake cha awali na cha sasa, huku akishindwa kuzitolea maelezo.

 

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga,Leonard Aloys na Yasin Katera.

 

 

Leave A Reply