The House of Favourite Newspapers

Mlela anaswa na mrembo

UTAWAAMBIA nini watu! Mwigizaji kunako kiwanda cha filamu Bongo, Yusuph Mlela amenaswa na mrembo mpya na baada ya kubanwa ameomba mpenzi wake wa sasa, Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ amvumilie tu. Mlela alinaswa na mrembo huyo juzikati kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa staa wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel ambapo alipobanwa kama ni shemu mpya mjini, alisema ni rafiki yake tu.

“Unajua Ebitoke asipojikaza atakuwa hajielewi kabisa kwa sababu nina marafiki wengi wa kike, hivyo ajikaze tu na akinifuatilia anaweza kujinyonga,” alisema Mlela.

IMELDA MTEMA, DAR

Comments are closed.