The House of Favourite Newspapers

Mlipuko Watikisa Jiji la Riyadh Saudi Arabia

0

MLIPUKO mkubwa leo (Jumanne) umelitikisa jiji la Riyadh, ikiwa ni siku tatu baada ya nchi hiyo kulikwamisha angani kombora lililokuwa likipita juu ya jiji hilo.

 

 

Hapakuwa na taarifa ya mara moja kutoka serikali ya Saudi Arabia, ambayo imekuwa ikishambuliwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani kutoka kwa waasi wa Huthi walioko katika nchi jirani ya Yemen tangu 2015.

 

Mlipuko huo ulitingisha madirisha katika jiji hilo, kwa mujibu wa waandishi wa habari na wakazi wake ambapo kuna habari pia kwamba mlipuko  miwili ilisikikia.

 

 

Jumamosi iliyopita, muungano wa wapiganaji unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unaunga mkono serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa dhidi ya wapiganaji wa Huthi, ulisema ulikwamisha kombora moja lililokuwa linaelekea Riyadh, kwa mujibu wa televisheni ya serikali.

 

 

Taarifa fupi iliyotolewa haikueleza chanzo cha mlipuko huo na wapiganaji wa Huthi wamesema hawahusiki.  Vilevile, Uwanja wa Ndege wa Mfalme Khaled jijini Riyadh umesema safari kadhaa za ndege zilifutwa kutokana na tukio hilo la Jumamosi.

 

Saudi Arabia imeongoza harakati za  kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Huthi tangu 2015 ambapo nayo imekuwa ikilengwa katika mashambulio kadhaa kutoka mpakani.

 

 

Leave A Reply