The House of Favourite Newspapers

Mmiliki wa Shule Mahakamani kwa Tuhuma za Mauaji ya Mwanafunzi

0
Viongozi wakiwa katika eneo la tukio ulipokutwa mwili huo.

MMILIKI wa Shule ya Msingi na Sekondari ya Scolastica iliyopo mji wa Himo wilayani Moshi, mkoani kilimanjaro, Edward Shayo amefikishwa mahakamani leo Jumatatu kusomewa shitaka la mauaji.

Shayo na watuhumiwa wenzake wawili watasomewa shitaka la mauaji ya mwanafunzi wa shule hiyo, Huphrey Makundi (16) wa kidato cha pili.

Mwili huo ukifukuliwa.

Mtuhumiwa ametolewa hospitali ya rufaa ya KCMC alikolazwa na kupelekwa moja kwa moja Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ambapo muda wowote atasomewa shtaka hilo pamoja na mlinzi wa shule na mwalimu mmoja ambao tayari nao wapo chumba cha mahabusu cha Mahakama.

Mtoto huyo alitoweka shuleni Novemba 11 na baadaye kubainika ameuawa ambapo maiti yake iliokotwa Mto Ghona, umbali wa mita 300 kutoka shule hiyo na kuzikwa kama ya mtu asiyefahamika, baadaye kufukuliwa Novemba 17.

Leave A Reply