The House of Favourite Newspapers

Mmoja wa Wenye Hisa Jamii Media, Mike Mushi Naye Ahojiwa na Polisi

0

mike-mushi

DAR ESA SALAA: JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemhoji mmoja wa wenye hisa katika Kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa.

Chanzo cha habari hii kimedai kuwa huenda Mike akaunganishwa na kesi mojawapo kati ya zinazomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Maxence Melo ambayo itatajwa Februari 16, 2017. Baada ya kuhojiwa, Mike ameachiliwa kituoni hapo kwa dhamana.

Maxence Melo anashtakiwa kwa makosa matatu ikiwemo kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao na Kusajili tovuti ya JF kwa domain ya .com badala ya .co.tz jambo ambalo Serikali inadai ni kinyume cha sheria.

CREDIT: JAMIIFORUMS

Leave A Reply