The House of Favourite Newspapers

Mnyarwanda Yanga Awapiga Biti AS Vita

 

STAA mpya wa Yanga, Issa Bigirimana, raia wa Rwanda amefunguka kuwa anawajua wapinzani wao AS Vita wanaotokea DR Congo huku akijipanga kuwaonyesha watakapokutana Agosti 4.

 

Bigirimana ni miongoni mwa mastaa wapya wa Yanga ambao watakuwepo kwenye mchezo wa kirafiki kati ya timu hizo ambao utapigwa Agosti 4, katika kilele cha Siku ya Mwananchi.

 

Bigirimana ambaye ametua na staa mwingine raia wa Rwanda, Patrick Sibomana, amesema kuwa siyo mara yake ya kwanza kucheza na Vita ambapo wapinzani wao hao wanamjua huku akijiandaa kuwaonyesha kazi.


“Hii siyo mara ya kwanza kucheza na AS Vita, wachezaji wengi wananifahamu sana kutokana na kukutana nao huko nyuma. “Siku hiyo ambao nitakutana nao Uwanja wa Taifa, Dar kwenye mechi hiyo basi nitawaonyesha kazi,” alisema Bigirimana.

Comments are closed.