The House of Favourite Newspapers

Mo Ibrahim wa Simba Afiwa na Mtoto Wake

 

Kiungo wa klabu ya Simba, Mohammed Ibrahim.

Kiungo wa klabu ya Simba, Mohammed Ibrahim amepata pigo jana baada ya kumpoteza mtoto wake wa kiume aliyefariki dunia

Klabu ya Simba pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wameungana na Watanzania wengine kumpa pole kiungo wao kwa pigo kubwa alilopata kumpoteza mtoto wake wa kiume ambaye bado alikuwa mdogo.

“Klabu ya Simba inatoa pole kwa kiungo wetu ‘Mohammed Ibrahim’ kwa kufiwa na mwanae mpendwa, tumeumia sote kwa msiba huu wa mtoto wetu mdogo kabisa. Klabu ya Simba inatoa pole kwa msiba huu mzito kwako na kwa famila nzima. Inna lillah wainna ilaihi Raajiun” alisema taarifa ya Simba

Comments are closed.