The House of Favourite Newspapers

FT: KUTOKA UWANJA WA TAIFA; SIMBA 1-0 AZAM FC

MPIRA UMEKWISHAAAAAA

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 90 Agyei anaingia vizuri, mpira unachukuliwa vizuri kabisa na Mlipili ndani ya 18, Azam wanasema faulo, mwamuzi anasema twende
Dk 88 krosi nzuri ndani ya lango la Simba, Manula anaokoa vizuri
Dk 86, Azam wanapata kona, inachongwa na Agye, Simba wanaokoa. Kotei yuko chini
Dk 85, Asante anaamua kujaribu akiwa mbali, lakini shuti lake linatoka mbaaali
SUB Dk 84 Simba wanamtoa Okwi na nafasi yake inachukuliwa Gyan
KADI Dk 82, Manula analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 76, Azam wanaingia vizuri lakini Arthur anaonekana ameotea

Dk 73, Kichuya nje ya 18, anaachia mkwaju mkali kabisa goal kick
SUB Dk 71, Yahaya Zayd anatoka na Mgahan Benard Arthur anaingia kuchukua nafasi yake
Dk 70 Abalora anaonyesha yuko vizuri , anapangua kichwa cha Okwi na kuwa kona ambayo hata huvyo haina manufaa
SUB Dk 69 Simba wanamtoa Ndemla na nafasi yake inachukuliwa na Muzamiru Yassin
KADI Dk 69 Amoah analambwa kadi ya njano kwa kumuagisha Okwi
Dk 67, mabeki Azam FC wanajichanganya wakati Yahaya akirudisha mpira lakini Okwi anachelewa na Morris anaokoa

Dk 66, Okwi anaingia vizuri lakini pasi yake kwa Kichuya inakuwa si nzuri, anajaribu krosi, Bocco anaruka tik tak lakini haina nguvu
Dk 64, Okwi yuko chini pale baada ya kuangushwa na Morris, lakini Azam FC ndiyo wanaonekana kumiliki zaidi mpira hasa eneo la kiungo
Dk 60 mpira sasa unamilikiwa zaidi na Azam FC na wanaonekana kupanga mashambulizi mengi zaidi kuliko Simba

KADI Dk 57, Asante naye analambwa kadi ya njano kwa mchezo usi sahihi
SUB Dk 55, Azam wanafanya mabadiliko mengine, anaingia Sure Boy kuchukua nafasi ya Kipwagile
KADI Dk 52, Okwi naye analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe

KADI Dk 50, Mkude analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe
Dk 49 mkwaju wa Chilunda unapita sentimeta chache katika lango la Simba, ilikuwa hatari, bahati kwa Simba, bahati mbaya kwa Azam

Dk 48, mkwaju mkali wa adhabu wa Okwi, kipa anatema na kuuwahi
KADI Dk 46 Morris analambwa kadi ya njano kwa kumgonga Bocco kwa makusudi
SUB Dk 45, Azam FC wanaaanza na mabadiliko, anatoka Yusuf nafasi yake inachukuliwa na Shabani Chilunda

GOOOOOOOOOO Dk 36, krosi safi ya Asante na Okwi anamshukuru Asante kwa kuitumbukiza wavuni vizuri kabisa
Dk 33, Simba bado wanashambulia zaidi na wanaonekana kuwazidia sana Azam Fc hasa katikati, wanapaswa kuwa makini

Dk 28 nafasi nyingine nzuri kwa Simba, Okwi anaachia mkwaju wa kimo cha nyoka, unakuwa goal kick, umetoka sentimeta chache kabisa
Dk 26 shambulizi jingine la Simba, krosi ya Asante, Bocco anaruka juu na kupiga kichwa, goal kick
Dk 25, Kapombe anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga baada ya Kapombe kuachia mkwaju mkali ndani ya 18 lililopita juu mtambaa wa panya
Dk 23, Okwi mara nyingine, anageuka na kuachia mkwaju mkali kabisa, kipa anadaka vizuri
Dk 21 Okwi anawatoka Kangwa na Kingue, lakini Kingue anatoa na kuwa kona, inachongwa na Kichuya, kipa anadaka vizuri kabisa.

Dk 20 Okwi anaruka kupiga kichwa anagongana na kipa Abalora na kuwa faulo

DK 18, Ndemla anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, mabeki wanazuia, unaokolewa
Dk 15, Kapombe anambabatiza Kangwa, mpira unakwenda nje na kuwa kona ya tatu kwa Simba. Inachongwa na Kichuya, hakuna kitu, kona butu
Dk 14, Manula anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kona wa Agyei, anauwahi tena, Agyei anaachia mkwaju mkaligoal kick
Dk 13, Mlipili anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira safi wa Mbaraka na kuwa kona, yuko chini pale anatibiwa
Dk 12, Okwi anageuka na kuachia mkwaju mkali, unaokolewa

Dk 10 sasa, Simba wanaonekana kulimiliki vizuri zaidi eneo la katikati ya uwanja, Azam FC inabidi watulie au wafanye mabadiliko ya kuangalia eneo hilo

Dk 5, Okwi anageuka ndani ya 18 kuachia mkwaju mkali kabisa, Abalora anadaka vizuri
Dk 5, Kipagwile anaruka na kupiga kichwa safi krosi ya Kangwa
Dk 3, Kona inachongwa na Ndemla, Abalora anapangua tena, wanaokoa
Dk 2, Simba wanapata kona, inachongwa na Kichuya, kipa anapangua inakuwa kona tena
Dk 1, mechi imeanza kwa kasi kubwa na kila timu inaonekana imepania kupata bao la mapema

KIKOSI CHA AZAM

1. Razak Abalora
2. Daniel Amoah
3. Bruce Kangwa
4. Yakubu Mohammed
5. Aggrey Morris
6. Stephan Kingue
7. Iddi Kipagwile
8. Frank Domayo
9. Mbaraka Yusuph
10. Yahaya Zayd
11. Enock Agyei
AKIBA
Mwadini
Mwantika
Abdallah
Salmin
Benard
Sureboy
Shabani

Comments are closed.