The House of Favourite Newspapers

Morocco, Hispania na Ureno Kuandaa Kombe la Dunia 2030 Kwa Pamoja

0

Marais wa vyama vya mpira wa miguu vya Morocco, Ureno na Hispania asubuhi ya leo Jumatano, Agosti 18, 2023 wamekutana jijini Lisbon, Ureno kujadiliana namna ya kuomba zabuni ya pamoja ya kuandaa Kombe la Dunia la mwaka 2030.

Mkutano wa viongozi hao umewakutanisha Fernando Gomes, Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Ureno, Fouzi Lekjaa, Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Morocco na Pedro Rocha, Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Hispania.

Viongozi hao wamekutana ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya kampeni inayounganisha mabara mawili kuandaa kombe la dunia, jambo linalotarajiwa kuweka historia mpya katika ulimwengu wa soka.

Hii ni mara ya pili kwa marais wa vyama hivyo vitatu vya soka kukutana, mara ya kwanzani ikiwa ni muda mfupi baada ya uamuzi wa FIFA kuhusu Kombe la Dunia la mwaka 2030 kutangazwa.

Katika mkutano huo uliofanyika Cidade do Futebol, Makao Makuu ya Shirikisho la Soka la Ureno (FPF), imeazimiwa kuwa nchi hizo ziwasilishe barua ya pamoja Oktoba 28, 2023 kwa FIFA kuonesha nia ya kuandaa Kombe la Dunia, hivyo kutimiza moja ya mahitaji ya mchakato wa maombi.

Hii itakuwa hatua ya kwanza rasmi kuelekea kwenye maombi ya zabuni hiyo ya pamoja kati ya nchi hizo tatu kuandaa Kombe la Dunia 2030.

Zoezi hilo la kihistoria, litafanyika Rabat, Morocco na kufuatiwa na mkutano na waandishi wa habari ambapo marais wa vyama hivyo vitatu vya mpira watashiriki.

Wakati huohuo, kamati ya zabuni ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2030, imeendelea na kazi yake ambapo Jumatano hii, huko Madrid, Hispania ilifanya mkutano mwingine wa kufuatilia mradi huo.

Leave A Reply