The House of Favourite Newspapers

Moto wa Mckinney Waenea kwa Kasi Kaskazini mwa Jimbo la Califonia

0
Moto umeacha madhara makubwa katika maeneo mbalimbali jijini California

MAMIA ya wazima moto huko California wapambana na Moto mkubwa zaidi wa Mwituni unaoendelea kuenea katika Jimbo la Kaskazini Nchini Califonia ulioanza siku ya Ijumaa.

 

Moto huo wa Mckinney ulianza Kaskazini mwa Kaunti ya Siskiyou siku ya Ijumaa,hadi kufia sasa tayari umeshateketeza Hekta 21,000 (ekari 52,500), huduma ya zima Moto ya Serikali ilisema. Takribani Wakazi 2,000 pamoja na wasafiri kwenye njia ya kupanda Mlima Pacific Crest wameodoka katika eneo hilo, pia mamlaka zimesema kuwa Nyumba zimearibiwa.

 

Onyo la Bendera Nyekundu inaonyesha tishio la hali ya hatari, huku California ikiwa inaendelea kukabiliwa na hali ya Ukame. Hali ya hatari katika Jimbo la siskiyou ilitangazwa siku ya Jumamosi baada ya Nyumba kuaribiwa Pamoja na Miundombinu

 

Gavana wa Jimbo hilo Anayejulikana kwa jina la Gavin Newsom alinukuliwa akisema kuwa:

Moto mkali unaendelea kuwaka kwa kasi kubwa

“Moto huo uliimarishwa na kuenea kwa nishati kavu, hali ya ukame uliokithiri, Joto kali, Upepo na Dhoruba za Umeme”

 

Mamlaka zinaonya kuwa huenda mvua za radi zinaweza kusababisha moto zaidi katika siku zijazo, Pia Huduma ya Misitu ya Marekani imeonya kuwa hali inaweza kuwa hatari sana.

 

Mtaalamu wa hali ya hewa Brad Schaaf aliliambia Gazeti la New York Times kwamba Moshi kutoka kwa Moto wa Mckinney unaweza kupunguza viwango vya Joto, ambavyo vinaweza kukabiliana na viungo hatari vya Radi.

Timu ya uokoaji inaendelea na juhudi za kuzima moto

California, bado inakabiliwa na hali mbaya ya ukame, mabadiliko ya hali ya hewa yanaongeza joto kavu, ambayo inaweza kusababisha kungezeka kwa moto wa Nyika.

 

Dunia imeongezeka kwa Takribani 1.1C tangu enzi ya viwanda ianze na hali ya Joto itaendelea kuongezeka, isipokuwa Serikali Ulimwenguni kote zikifanya upungufu katika uzalishaji wa viwanda.

Leave A Reply