The House of Favourite Newspapers

Moto Wateketeza Makumbusho Kongwe ya Miaka 200 Brazil

makumusho

KIKOSI cha zimamoto nchini Brazil kinajaribu kuzima moto mkubwa uliotokea katika moja ya makumbusho kubwa na ya kihistoria mjini Rio De Jeneiro.

Picha za televisheni zinaonesha makumbusho hiyo ikiteketea kwa moto.  Makumbusho hiyo inakadiriwa kuwa na miaka 200 na ina mamilioni ya vitu vya historia ikiwemo mifupa ya mwanamke wa kale zaidi kugunduliwa huko Marekani. Makumbusho hiyo inakadiriwa kuwa na vitu milioni 20, haijajulikana bado kama kuna marejuhi yeyote.

Chanzo cha moto bado kinachunguzwa na mamlaka nchini Brazil. Mapema mwaka huu makumbusho hiyo ilisherehekea kutimiza miaka 200. Rais wa Brazil katika ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa, imekuwa siku ya huzuni kwa Wabrazil wote, na kuharibika kwa jengo hilo hakuwezi kufananishwa na thamani ya historia iliyopotea.

Naye mkurugenzi wa Makumbusho amesema kuwa ni tukio la kusikitisha sana.  Kwa mujibu wa tovuti ya kituo hicho, ndani yake kulikuwa na vitu mbalimbali vya historia ya Brazil na nchi nyingine ikiwemo Misri.

Sehemu muhimu ya historia iliyopotea katika jengo hilo ni pamoja na mifupa ya watu wa kale ikiwemo mifupa ya mwanamke wa kale kutoka Marekani ambayo ina miaka elfu kumi na mbili na mifupa ya waliokuwa wanyama wakubwa zaidi duniani maarufu kama dinosaur. Wafanyaki wa makumbusho hiyo waliwahi kuripoti kutokuwepo kwa bajeti ya kutosha na kusahaulika kwa jengo hilo.

Comments are closed.