Moto Wazidi Kuwaka Shigongo Cup, Nyanzenda FC Yatinga Hatua ya Nusu Fainali
Mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya mashindano ya Shigongo Cup yanayoendelea Buchosa umepigwa kati ya Nyanzanda FC dhidi ya Bugoro FC ambapo Nyanzenda imefanikiwa kusonga mbele na kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Bugoro mabao 3-0.
Mabao ya Nyanzenda yamefungwa na Msonda James katika dakika ya 56, Amos Chrispiano dakika ya 71 na Denis Kadushi dakika ya 82.
Kocha wa Nyanzenda, amenukuliwa akisema mipango yake ilikuwa ni kushambulia kwa kushtukiza, mbinu iliyompa ushindi huo.
Kwa upande wake, nahodha wa Bugoro amesema mashindano hayo yamekuwa na mvuto mkubwa kwa vijana na kueleza kuwa licha ya timu yake kupoteza mchezo huo, wanamshukuru mbunge wao, Eric Shigongo kwani mashindano hayo yameleta hamasa kubwa na kuomba yawe endelevu.