The House of Favourite Newspapers

Updates: Prof . Mbarawa Aunda Tume Kuchunguza Chanzo cha Moto Uwanja wa Ndege Dar

airport

 

DAR ES SALAAM: Moto mkubwa umezuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa leo na kusababisha taharuki kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, ambapo imelazimu shughuli zote uwanjani hapo kusitishwa kwa muda wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.

vlcsnap-978548

Moto ukiwaka viwanjani hapo.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno ameuambia mtandao wa Global Publshers kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za kawaida zinaendelea kama kawaida.

moto

Wasafiri wakitaharuki kuona moto huo ukizuka na kusababisha taharuki kubwa miongozni mwao.

Aidha Meneja wa Uwanja huo Bw. Paul Rwegasha ameeleza kuwa kwa sasa shughuli zote za usafirishaji zimehamishiwa Terminal One na zinaendelea kama kawaida huku wakiweka sawa maeneo yalioathirika.

“Kwanza naomba niwatoe hofu Watanzania na wasafiri wote wanaotumia Uwanja wetu, ni kweli moto umezuka kuanzia majira ya saa 6 hadi saa 7 usiku wa kuamkia leo.

moto1Raia akichukua picha za tukio hilo huku walinzi wakitaharuki.

“Lakini madhara kidogo yametokea kwenye jengo la kuhifadhia mizigo pekee, hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto, mashine zote zipo salama na sasa shughuli zote za usafirishaji tumezihamishia kule terminal one (Uwanja wa zamani) zinaendelea, ndege zote kubwa na ndogo zinaruka na kutua kama kawaida”. Amesema Meneja huyo.

moto2Vikosi vya ulinzi na usalama vikiwasili eneo la tukio.

“Baada ya kuudhibiti moto huo tumerudi kuangalia chanzo tumekuta, mfumo wa umeme uko sawa, hivyo hatujajua chanzo hasa cha moto huo ila tunajitahidi kufanya utafiti ili tujue.” Aliongeza Meneja na kusema taarifa zaidi, zitatolewa baadaye.

 

UPDATES: CHANZO CHA MOTO UWANJA WA NDEGE DAR CHAJULIKANA

Taarifa zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, chanzo cha moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salam na kusababisha shughuli zote za usafirishaji Uwanjani hapo kusimama kwa muda, kimejulikana kuwa ni hitilafu ya umeme.

Akizungumza na mtandao wa Global Publshers mapema asubuhi ya leo, Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno amesema kuwa, uchunguzi umebaini kwamba, kulikuwa na tatizo la umeme ambalo hata hivyo lilishughulikiwa mara moja.

“Kulikuwa na tatizo la umeme kwenye eneo la kuhifadhia mizigo lakini moto ulidhibitiwa vizuri na sasa shughuli zinaendelea kama kawaida japokuwa bado tunatumia Terminal One (uwanja wa zamani) kwa kuwabeba abiria kwenye mabasi na kuwapeleka panapohusika.

“Kwa sasa ndege zote zinatua na kuruka bila tatizo lolote na kufuatana na ratiba hivyo hakuna hofu yoyote kwani muda si mrefu eneo hilo la mizigo litakuwa limeshawekwa sana, ” alisema Kamanda Otieno.

Aidha Mamlaka ya Uwanja huo imetoa mabasi kwa ajili ya kubeba abiria kuwapeleka Terminal One ambako shughuli za usafirishaji zinaendelea kama kawaida.

UPDATES: HUDUMA ZA UFAFIRI KATIKA UWANJA WA NDEGE DAR, TERMINAL 2 ZAREJESHWA KAMA KAWAIDA BAADA YA TAHARUKI YA MOTO

Hudua za usafirishaji abiria katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA), Terminal 2 zimerejeshwa kama kawaida baada ya taharuki kufuatia kuibuka kwa moto mkubwa uliozuka usiku wa kuamkia leo  na kusababisha huduma hizo kufungwa kwa muda na kuhamishiwa Terminal 1.

Hii hapa taarifa ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege iliyotolewa kupita Twitter ya Precision Air..

jnia

 

 

Updates: Tume yaundwa kuchunguza chanzo cha moto uliotokea Uwanja wa ndege wa JNIA

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameunda tume ya watu 12 ili kuchunguza chanzo cha moto uliotokea katika chumba kinachotumika kuhifadhia mizigo ya abiria wanaotoka nje katika Uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JNIA)  Terminal two.

Aidha Prof Makame ametoa muda wa mwezi mmoja kuangaliwa kwa makini utendaji wa kampuni ya Swissport.

Prof. Makame Mbarawa mapema leo hii alitembelea sehemu ya uwanja huo wa ndege na kujionea madhara yaliyosababishwa na moto uliotokea usiku wa kuamkia leo ambapo amesma kuwa mara baada ya kujua chanzo cha moto huo basi watajipanga vema ili kuhakisha madhara kama hayo hayatokei tena katika viwanja vya ndege.

Mwandishi Wetu/ GPL

Comments are closed.