The House of Favourite Newspapers

Mourinho: Ibrahimovic, Lingard wameniangusha

0

KOCHA Jose Mourinho amewalalamikia washambuliaji wake wa Manchester United wakiwemo Zlatan Ibrahimovic na Jesse Lingard, kuwa ni sababu ya wao kushindwa kupata ushindi katika mchezo wa Robo Fainali ya Europa League dhidi ya Anderlecht usiku wa kuamkia jana.

Man United iliongoza kwa bao 1-0 muda mrefu na kujipa matumaini kuwa itamaliza mchezo huo ikiwa na ushindi, bao hilo lilifungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika ya 37 lakini mambo yalibadilika na wapinzani waowakasawazisha kupitia kwa Leander Dendoncker katika dakika ya 87.

Dendoncker alifunga kwa kichwa likiwa ni shambulizi la kwanza kupigwa mpira uliolenga lango kwa wenyeji hao,
jambo ambalo Mourinho ameliita ni uzembe wa washambuliaji wake kushindwa kumalizia kazi nzuri wanazofanya.
“Tunatakiwa kumaliza mchezo mapema, tulikuwa na nafasi, tulimiliki mpira, lakini hatufungi mabao, kulikuwa na nafasi nyingi za kuumaliza mchezo mapema, hatufanyi hivyo kwa kuwa ni uzembe uliofanyika katika sehemu ya ushambuliaji wetu.

“Kwa aina ya wachezaji tulionao hatuhitaji mbwembwe nyingi kumaliza kazi, tunaye (Marcus) Rashford, (Jesse) Lingard, (Zlatan) Ibrahimovic, (Anthony) Martial wote walicheza soka la kufanana. “Lakini waliocheza nyuma yao walikuwa imara, mabeki nao walifanya kazi nzuri, tulitakiwa kucheza mechi ya marudio Old Trafford tukiwa mbele,” alilalama Mourinho.

Kwa Man United sare hiyo ni ya 14 katika michuano yote tangu kuanza kwa msimu huu ambapo aliwataka mabeki kuwa na hasira wanapoona washambuliaji wao hawafanyi kazi inayotakiwa. Nahodha wa Man United, Michael Carrick alimuunga mkono kocha wake kwa kusema walitakiwa kuumaliza mchezo mapema.

Leave A Reply