The House of Favourite Newspapers

Moyo Sukuma Damu: Hazina Iliyofichwa Maktaba Mwaka Mzima!

   ditto2 Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erik Evarist (wa kwanza kulia) akimuonyesha Lameck Ditto (katikati) utengenezaji wa gazeti la Championi kwa msanifu kurasa, Noel.

Makala: Erick Evarist, Gazeti la Risasi Jumamosi, Toleo no. 1393, Januari 21-24

MOYO Sukuma Damu ndio habari ya mjini. Ni wimbo ambao unawafariji watu wengi kwa sasa. Utunzi wake umewachoma watu ambao walikuwa wana maumivu ya mapenzi. Umewaponya majeraha waliokuwa na majeraha yao yale ya muda mrefu na hata yale ya muda mfupi.

ditto-8

Msanii aliyepikwa vyema na Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Lameck Ditto.

Wimbo umewapa ujasiri wa kusema, ‘acha niachane naye maana sikuzaliwa naye’. Wengi wameiambia mioyo yao ifanye kazi ambayo Mungu alikusudia ifanye, kusukuma damu. Maumivu ya mapenzi tupa kule.

Wimbo umebeba maana pana sana ya mapenzi. Na huo si utunzi wa mtu mwingine bali ni msanii aliyepikwa vyema na Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Lameck Ditto ambaye hapa chini amezungumza mengi kuhusiana na muziki wake.

Mikito Nusunusu: Moyo Sukuma Damu ni wimbo mzuri, unafikiri una utofauti gani na nyimbo zako nyingine zote zilizotangulia?

ditto-5

Mhariri Msadizi wa Gazeti la Ijuamaa, Andrew Carols akijiachia na Ditto.  

Ditto: Tofauti ipo kwenye namna nilivyouimba, nilivyouandika na namna ulivyopokelewa. Umenisaidia kuongeza idadi kubwa ya mashabiki, namshukuru Mungu kwa hilo. Na umeonesha dalili za kuendelea kukua kwa thamani ya muziki wangu.

Mikito Nusunusu: Ulitumia muda gani kuuandika?

Ditto: Nilikaa na wazo la wimbo muda mrefu. Inaweza kufika takriban mwaka mmoja ingawa kwenye kuandika                        wimbo kupitia wazo hilo sikutumia muda mrefu sana.

Mikito Nusunusu: Mbali na ngoma hii, ngoma gani nyingine ambayo kwako wewe ni kali kwa miaka nenda rudi.

Ditto: Ngoma nyingi ambazo nimezifanya kwangu ni nyimbo nzuri na zote nazipenda, kwa sababu kila moja ilifanya vizuri kwa nafasi yake, kila moja ilichukua nafasi yake ikafanya vizuri ikakubalika na kila mtu so nazipenda zote kuanzia ile Dunia ina Mambo, Tushukuru kwa Yote, Wapo, Ulibisha Hodi zile nilizofanya zamani kila moja ilikuwa na nafasi na uzuri wake.

ditto-1

Lameck Ditto (kushoto) akiongea na Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kulia).

Mikito Nusunusu: Unapoitazama THT unaona nini? Ina mchango gani katika muziki wako?

Ditto: Mchango wa THT ni mkubwa sana, nadhani nashindwa hata kuupima kwa kuulezea. THT ndio walionisaidia kujenga msingi wa ninachokifanya. Lakini pia knowledge nyingi za kimuziki na kila kitu ambacho nakifanya. Vitu vingi nilikuwa sivijui nimevijua pale kwa maana ya kupewa maarifa. THT ndio imebadilisha kila kitu changu, maisha yangu yamebadilika kupitia THT.

Mikito Nusunusu: Muziki umekupa mafanikio gani ya kujivunia hadi sasa?

Ditto: Mafanikio ni mengi sana kwa muda wa miaka karibia mitano sasa muziki unaendesha maisha yangu. Kwa maana ya kila kitu nilichokuwa nacho. Nina kila kitu ambacho kijana wa umri wangu anatakiwa kuwa nacho. Na nimejenga msingi mzuri wa ninayoyafanya sasa na nitakayoendelea kuyafanya baadaye. Sipendi sanaa kuzungumza mafanikio by the way.

ditto-6

Mikito Nusunusu: Unazungumziaje wasanii wanaofanya muziki kwa kutegemea kiki zaidi kila wanapoachia ngoma maana wengi siku hizi hawatoi ngoma bila kufanya jambo.

Ditto: Siioni kama hiyo ni njia mbaya. Wanaofanya kiki za hapa na pale kubusti muziki wao, wanafanya hivyo kwa malengo yao na ninaamini wanayafikia. Mimi kwa upande wangu, muziki wenyewe unaongea, sina haja ya kiki za aina yoyote.

Mikito Nusunusu: Unapomtazama Afande Sele sasa hivi unajifunza nini kutoka kwake?

Ditto: Nikimtazama Afande Sele (Seleman Msindi, mkongwe wa Bongo Fleva) naona mtu ambaye ana muwezo mkubwa wa muziki, ana kipaji kikubwa ana heshima kubwa na amejaribu kufanya kazi kubwa kwa ajili ya muziki wetu. Na sisi wenyewe na amekuwa ni kielelezo  cha muziki wetu na kwa muda sasa umefika hata miaka  17 kama si 18 mtu ambaye ameimarika zaidi. Amekuwa na nguvu ile ile aliyokuwa nayo mwanzo.

Ni mtu ambaye namuona ana heshimika sana. Aliyefanya vitu ambavyo vitakumbukwa na vizazi na vizazi. Namtazama Afande kama Icon ya muziki. Icon ya vijana, Icon ya watunzi. Najifunza mambo mengi kutoka kwake, kwaza kuhakikisha unapotunga kazi zako ziwe ni kazi ambazo zitafikirisha watu wengine yani mtu akisikia, atafikiria. Leo hii ukisikiliza Darubini Kali unainjoi mpapa sasa, Wacha Kupiga Mayowe, Mkuki Moyoni, najifunza namna yake ya utungaji na ndio alama aliyoiweka Afande Sele.

ditto-11

Mikito Nusunusu: Hujaoa, una mpango gani.

Ditto: Hilo lina muda wake maana hata maandiko yanatufundisha hivyo muda wake ukifika, litafanyika. Nina mpenzi wangu ambaye ndiye nimezaa naye mtoto mmoja na ndio huyo Mungu akipenda nitamuoa.

Mikito Nusunusu: Mke wako hasumbui unapotoka usiku kwa shuguli za muziki?

Ditto: Hasumbui, anaelewa kwa sababu si ndio kazi. Nipo naye muda mrefu kwake yeye sio tatizo hata kidogo. Anasapoti ninachokifanya na anaelewa kazi  zetu za muziki zinazofanyika lakini pia ananiamini sana. Nyinyi wenyewe (Global Publishers) mimi ningekuwa ‘kwatukwatu’ mngekuwa mshanijua tu hahaha…mimi tunaaminiana na tunaheshimiana, hajawahi kusumbua popote kuhusiana na kazi yangu.

Mikito Nusunusu: Plan zako kwa mwaka huu ni kuachia ngoma ngapi hadi tunaifunga Desemba maana huwa unachelewa sana kuachia ngoma mpya.

Ditto: Itategemea na nyimbo ambazo natoa. Bado sina kiasi ambacho naweza kusema nitatoa mwaka huu ila sasa hivi hatutachelewa sana, tutaangalia  mazingira yatakavyoruhusu.

Mikito Nusunusu: Prodyuza gani unamkubali sana Bongo na ni kwa nini?

Ditto: Maprodyuza wote, nakubaliuana nao kwa sababu kila mmoja naona ana kitu fulani kinanivutia hivyo mimi naona wote wanafanya vizuri.

Comments are closed.