The House of Favourite Newspapers

Mr Blue: Hatukuwaza Kupiga Pesa

0

MR BLUE a.k.a Byser au Babylon Bizz; ni rapa bora wa wakati wote nchini Tanzania ambaye anasem  Eenzi hizo wakati wanaanza kufanya muziki hawakuwaza kufanya hivyo kwa ajili ya kupiga pesa tofauti na ilivyo sasa.

 

Byser; akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, anasema kuwa, siku hizi mtu anatamani kuwa msanii ili apate pesa, lakini kwa upande wa wasanii wa zamani waliwaza kutngeneza ngoma zitakazodumu muda wote hivyo pesa zilikuja zenyewe baadaye.

 

“Siwakatazi wasanii wa sasa hivi kupiga pesa, lakini wakati wetu hatukuwaza kabisa suala la pesa, tuliwaza kutengeneza muziki mzuri utakaoacha alama na pesa zilifuata baadaye kwa sababu tuliamini muziki huu ukishakubalika, pesa zitakuja tu na hivyo ndivyo ilivyokuwa,” anasema Mr Blue; mmoja wa wasanii waliodumu kwenye gemu kwa muda mrefu na ana mafanikio makubwa.

 STORI; MEMORISE RICHARD

Leave A Reply