The House of Favourite Newspapers

Nandy: Sijagombana Na Wema

0

FAUSTINA Charles au Nandy The African Princes; ni malkia wa muziki Afrika Mashariki akiiwakilisha vyema Tanzania ambaye anasema kuwa, hajawahi kugombana na staa mwenzake Bongo, Wema Sepetu Isaac Sepetu na wala hajawahi kumchukulia bwana kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiongea.

 

Nandy au Nandera ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, kipindi cha nyuma kuna maneno mengi yalisambaa mitandaoni, kwamba yeye na Wema ni kama paka na panya kutokana na kile kilichodaiwa kwamba, eti wameibiana mabwana, jambo ambalo mwenyewe anasema halikuwa na ukweli wowote.

 

“Huwezi kuamini, mimi na Wema hatujawahi kugombana kabisa, nilikuwa nashangaa wanavyosema eti nilimuibia danga lake, kitu ambacho hakina ukweli wowote, siwezi kufanya hivyo, halafu kwa nini tuibiane? Kwani wanaume wameisha hapa mjini? Watu huwa wanaongea sana, halafu wanaongea mambo wasiyokuwa na uhakika nayo, nampenda Wema na sitaacha kufanya hivyo, zaidi tunasapotiana sana kwenye kazi,” anasema Nandy anayesubiria Juni 25, mwaka huu afunge ndoa na mchumba’ke, Billnass au Nenga.

Stori: Memorise Richard, Dar

Leave A Reply