The House of Favourite Newspapers

MR CHUZI KAMWE HANA MPANGO WA KUOA!!

WAKATI akiwa na watoto wanne aliozaa na mama tofauti, mwigizaji mkongwe wa Bongo Movies, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuzi’ ameibuka na kueleza kwamba kamwe hana mpango wa kuoa.

 

Akipiga stori na Za Motomoto News, Chuzi alisema kuwa, uamuzi wake ni kwamba hataoa hadi mwisho wa maisha yake na anachokifanya kwa sasa ni kuwalea watoto hao wanne alionao hivyo wanaosubiri aoe au waliotarajia awaoe, waandike maumivu.

 

“Sina mpango wa kuoa maishani mwangu, watoto wanne nilionao ambao ni Abdrahim, Abdmalick, Salma na Ahmed wananitosha. Kwa sasa natafuta fedha kwa kasi ili niwalee vizuri maana ndiyo kazi iliyobakia,” alisema Chuzi.

NA GLADNESS MALLYA | RISASI JUMATANO

Comments are closed.