The House of Favourite Newspapers

Mr Shinda Nyumba Apagawisha Ubungo, Kibamba na Kiluvya

Mr Shinda Nyumba akigawa vipeperushi katika mitaa ya Ubungo.

Mr Shinda Nyumba akigawa vipeperushi kwa wasomaji wa magazeti ya Global Publishers wa Ubungo.

Msomaji wa magazeti ya Global Christopher John mkazi wa Kibamba akijaza kuponi.

Msabaha Mohamed wa Kibamba akijaza kuponi mbele ya wasomaji wengine wa magazeti ya Global Publishers.

Issa Yusuph wa Kibamba akichana kuponi baada ya kujaza.

Mr Shinda Nyumba akimjazia kuponi msomaji wa magazeti ya Global Publishers.

Deborah Mbwana, mkazi wa Mbezi akijaza kuponi.

Rehema John msomaji wa magazeti ya Global ambaye ni mkazi wa Mbezi akijaza kuponi mbele ya dereva wa Global, Kefa Masaga.

Aman Godwin akiwa na Mr. Shinda Nyumba baada ya kujaza kuponi.

Mwamvita Ally mkazi wa Kibamba akijaza kuponi.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendelea kwa sasa chini ya Kampuni ya Global Publishers Ltd, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Amani, Ijumaa Wikienda na Risasi inazidi kusonga mbele.

Watu mbalimbali wanaendelea kujitokeza na kujaza kuponi kwa wingi ili kutengeneza nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kila mwezi zikiwemo pikipiki na simu za kisasa ili hatimaye wajishindie nyumba katika droo kubwa itakayochezeshwa hapo baadaye.

Huku bahati nasibu hiyo ikiendelea kuwa gumzo kutokana na msisimko iliyonayo, leo Mr Shinda Nyumba anayesepa na kijiji kila kona anakopita, alikuwa Mitaa ya Ubungo, Kibamba mpaka Kiluvya ambako kote amevuruga na kuacha gumzo.

Mbali na kumshangaa Mr Shinda Nyumba, wakazi wa maeneo hayo walijitokeza kwa wingi kununua magazeti na kujaza kuponi huku wakionesha dhahiri kupania kujishindia nyumba pamoja na zawadi mbalimbali.

Comments are closed.