The House of Favourite Newspapers

Mrembo Kutolewa Mahari Ng’ombe 500 Magari V8 Matatu!

Nyalong Ngong Deng Jalang (kulia).

MSICHANA Nyalong Ngong Deng Jalang hivi sasa anajitayarisha kutolewa mahari ya ng’ombe 500 na magari matatu aina ya Toyota V8.

Msichana huyo mwenyeji wa Sudan ya Kusini, amewaweka kwenye msululu wanaume watano wanaowania kumwoa ambapo mmoja aitwaye Kok Alat, anaongoza kwa kupendekeza mahari ya ng’ombe idadi hiyo na magari yaliyotajwa.

Miongoni mwa washindani wa kumwoa mrembo huyo ni mkuu wa zamani wa Wilaya ya Awerial na gavana wa sasa wa Jimbo la Eastern Lakes.

Pamoja na yote, swali linaloulizwa na watu wengi ni: Hivi huyu mwanamke ana nini ambacho wanawake wengine hawana?  Na, iwapo ungeungana katika mbio za kumwoa, ungetoa ng’ombe wangapi?

 

Comments are closed.